.

πŸ‘‰ Maelfu ya wakazi wa Mwanza wameuaga mwili wa Alphonce MawazoπŸ‘‡βœ”

IMG_20180125_210009.jpg

Imehaririwa na; Melkisedeck Leon Shine. Tarehe 29 Jan 2016 14:45. [Legal & Authority]


Maelfu ya wakazi wa Mwanza wameuaga mwili wa Alphonce Mawazo

3.png Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza,wakiongozwa na mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) Mh.Freeman Mbowe wameuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita Alphonce Mawazo,huku baadhi ya viongozi wa chama hicho,wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu wakilitaka jeshi la polisi mkoani Geita kuhakikisha watu waliohusika na mauaji ya kiongozi huyo wanakamatwa na kufikishwa mahakamani mara moja.

Tukio la kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza limetanguliwa na ibada iliyoongozwa na mchungaji Bernard Swai wa kanisa la Winners.

4.png
Fredrick Sumaye,waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu pamoja na aliyekuwa mgombea urais wa chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA ), Mh. Edward Lowassa wakatoa angalizo kwa jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linatenda haki katika kushughulikia kifo cha marehemu Alphonce Mawazo.

Mtoto wa marehemu Alphonce Mawazo,Precious Mawazo mwenye umri wa miaka tisa akatokea mbele ya halaiki kuelezea majonzi ya kufiwa na baba yake.

Mwenyekiti wa taifa wa Chadema Mh. Freeman Mbowe naye akatoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Alphonce Mawazo, aliyeuawa kikatili kwa kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu katika kijiji cha Katoro wilayani Geita.

Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo tayari umewasili mjini Geita ambako utalala usiku huu ili kutoa nafasi kwa wananchi wa mkoa huo kutoa heshima zao za mwisho siku ya jumapili asubuhi Novemba 29, kabla ya kupelekwa nyumbani kwao katika kijiji cha Chikobe kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya jumatatu Novemba 30.
2.png

Soma%20Zaidi.gif Napendekeza uendelee kusoma kuhusu; Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Chumvi.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Maelfu ya wakazi wa Mwanza wameuaga mwili wa Alphonce Mawazo).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Nini maoni yako kuhusu, Maelfu ya wakazi wa Mwanza wameuaga mwili wa Alphonce Mawazo? Niandikie hapa
Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
Kichekesho%20Kipya Namna ya Kukutana na Rafiki mliopotezana Unaweza kukuta na yeye anakutafuta
πŸ‘‰SOMA ZAIDI HAPA...Kizuri

IMG_20180108_172400.jpg

Ujumbe wangu kwako kwa sasa

"Kitu chochote kinapofanywa vizuri mwanzoni ni sawa na kimefanywa nusu tayari."

Slide2-utotoni.GIF

.

.

b.gif

Mimi ni Melkisedeck Shine Mmiliki, Mwandishi /Mhariri. Karibu tena kila siku.

MAWASILIANO | KUHUSU MWANDISHI

Blog nyingine maarufu ndani ya AckySHINE.com

| Vichekesho | Videos | Picha | Ujasiriamali | Mahusiano | Kilimo & Mifugo | Katoliki | Afya & Mapishi | Hadithi | Misemo | SMS