Kisa cha wizi mpya wa kwenye ATM 🏧 πŸ’³

Mdada mmoja ametusimulia kisa hiki..
Wapendwa kuweni macho…
Nilikua pale Total nje ya Mliman city nikaenda kutoa hela NBC nikakuta machine haitoi hela since ni master card nikaenda Atm ya CRDB..

Mule ndani alikuepo mdada kama mm mdogo kwa umbo looks naive.. Nikamuuliza hutoki? Akajibu endelea tu , mm natoa hela nyingi so nitawachelewesha ..
Akaendelea kuongea, halafu utoe card taratibu hii Atm ina tabia ya kukwaruza card..nikajibu sawa..

Nikafanya muamala kama kawaida..card ilivyotoka huku machine inahesabu hela akasogea akawa anaivuta card yangu..wakati mm nahesabu hela, nikashangaa lakini nikachukulia poa..nikaona anaitoa taratibu isikwaruzike ..Nikatoa hela nikapokea card toka kwake nikaondoka…

Nikawaza tu hajatoka coz Atm inatoa elfu 5 5 so note 40 ni laki 2 labda anatoa milioni coz alikua anahesabu pale…sikumjali na sikushtuka hata kidogo, nikaondoka.
Kesho yake nilisafiri kikazi kwenda Dodoma, stayed for 2 weeks hapo cjui km nilibadilishiwa card since siku access Atm Tena..

Basi nimerudi Dar naenda kutoa hela kila nikiweka password Naambiwa nakosea ,baadae card ikamezwa.. Nikaingia ndani bank wanitolee card iliyomezwa ,nikawaambia sio yangu.. wakasema hii pekee ndio imekutwa kuicheck kweli sio yangu..

Nikawatajia acc kuangalia miamala kibao imeshafanywa, wameiba 8m kumbe kila siku walikua wanatoa..
Wakanambia, alikariri password, na alipotoa kadi yako ,alikubadilishia na kukupa ya kwake aliyokuwa ameishika tayari mkononi..
Ndipo nikashtuka na kukumbuka, Nikawasimulia incidence yote, wakaniambia hakuna mwingine na wanamtafuta sana ameshaibia watu wengi kwa style ya kubadilisha card akishakariri password..

Wakanambia hakuna namna watanerefund coz ni kosa langu..ukiwa ndani ya ATM unatakiwa uwe peke yako nilipaswa nimwambie atoke…

Nami nikaona niwashirikishe huu wizi mpya wanaoutumia kwa Sasa..

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

ml.gif
UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG