Historia ya Kabila la Wanyaturu

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Mapishi ya Samaki wa kupaka, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Historia ya Kabila la Wanyaturu.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Historia ya Kabila la Wanyaturu

By, Melkisedeck Shine.

WANYATURU ambao awali walijulikana kwa jina la Warimi ni watu wanaoishi karibu wilaya zote za mkoa wa Singida yenye tarafa saba. Kwa Mujibu wa Patrick Mdachi katika kitabu cha Wanyaturu wa Singida, Mila na Desturi zao, Wanyaturu ni moja ya makabila yanayojumlishwa katika kundi la Nilo-Hamites, lenye asili ya Wabantu walioishi Abysinia ambayo sasa inajulikana kama nchi ya Ethiopia.

Watu hao waliihama Abysinia (Ethiopia) kutokana na njaa kubwa kiasi ambacho hawakuweza kustahimili kukaa tena hapo. Njaa ndiyo iliwalazimisha watu hao kufikia kula nzige, katika harakati za kutafuta nzige hao ndio ukawa mwanzo wa safari yao ya kuhama.
Mdachi anasema katika kitabu chake hicho kilichochapishwa na Benedictine Publicationss Nandanda - Peramiho mwaka 1991, kuwa Wanyaturu waliingia Tanzania kupitia sehemu ya kaskazini kutokea Kenya na Uganda na kufanya maskani yao eneo la Uzinza, Mwanza, baadaye walihamia eneo la Pasiansi na mwaka 1700 walikutwa na Wasukuma ambao waliwafukuza na kuwafanya wakimbilie Ntunzu. Baadhi ya watu hao (yaani Mwilwana na Masanja) wakiwa na wake zao na watu wengine wa kuwasaidia kazi hawakuweza kukaa Ntunzu, waliendelea na safari pamoja na ng’ombe wao mpaka mkoani Singida, eneo la mashariki lijulikanalo kama Sepuka.
Mdachi anasimulia kwamba Wanyaturu hao walikaa hapo kidogo na ndio eneo hilo ambalo watu hao waligawanyika tena, lengo likiwa ni kupeana nafasi ya kilimo, ufugaji na kuweka makazi ya kudumu. Mwilwana akielekea kaskazinimashariki eneo la Ilongero ambapo alistawisha makao yake hapo na hapo ukawa mwanzo wa Mwilwana huku Masanja akienda upande wa mashariki eneo la Kisaki na kujenga juu ya jiwe liitwalo Wahi, anasimulia Mdachi.
Kwa mujibu wa masimulizi hayo, Masanja alijaaliwa kuwa na watoto wanne ambao aliwapa majina yao kulingana na kazi walizofanya au tabia. Watoto hao ni Sengasenga aliyepewa jina hilo kutokana na kuwa baba yao alipoanza akiwa maskani alifyeka mapori. Kufyeka pori kwa Kinyaturu ni ‘Usenga’.
Mtoto mwingine aliyefuatia aliitwa Mpuma ambaye alipewa jina hilo kutokana na eneo hilo kuwa na tumbili wengi. Mpuma kwa Kinyaturu ni tumbili. Mtoto wa tatu alipewa jina la Hati kutokana na jiwe ambalo baba yao alitumia kujenga nyumba na wa mwisho alijulikana kwa jina la Mkahiu kutokana na furaha ya wazazi wao. Watoto hawa walitawanyika ikiwa ni suluhu ya ugomvi wao na kila mmoja alianzisha ukoo wake ambazo zilikuja kujulikana kama Senga, Anyahati, Puma na Ukahiu.
Utafiti unaonesha kuwa jina la kabila la Wanyaturu ni la hivi karibuni, awali kabila hili lilijulikana kama Warimi. Jina hilo walipewa na watani wao Wanyamwezi ambao walikuwa wakiwinda pamoja.
Siku moja wakiwa katika kuwinda walimpiga mshale wa sumu mnyama wa porini, mnyama huyo akakimbia na Wanyaturu wakiwa wanamkimbiza walikuwa wakisema ‘Mughuu turu, turu’ wakimaanisha mguu huu hapa.
Maandiki haya ni sehemu tu ya historia ya Wanyaturu..✍🏿

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Historia ya Kabila la Wanyaturu, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

tafuta-rafiki.gif
SALAMU-MPENZI-MCHANA-33097HG34MX.JPG