Historia ya Kabila la Wangoni

By, Melkisedeck Shine.

Wangoni ni moja ya kabila linalopatikana nchini Tanzania na baadhi ya maeneo mengine kusini mwa Afrika. Ni kabila ambalo lina historia ya aina yake kama ilivyo kwa makabila mengine ya kibantu hata yale yasiokuwa ya kibantu.

Kuna mambo mengi sana ya kuzungumzia juu ya kabila la Wangoni. Kwa kuwa tumesoma mengi na tumesikia mengi sana juu ya kabila hili la Wangoni. Hivyo Katika makala hii fupi napenda tujadiliane asili ya jina hili la Wangoni. Kwa nini Wangoni waliitwa Wangoni na je ni wapi hasa chimbuko la Wangoni.? Kwa mujibu wa maandiko ya Fr. Elzear na Ndugu Romanus Mkinga na masimulizi ya wazee wanasimulia kuwa,Historia na habari ya asili ya jin la Wangoni linaanzia kusini mwa Afrika.

Hapo awali hata kabla ya miaka ya 1000, kulikuwa na wakazi wa mwanzo wa Wazulu waliofahamika kwa jina la Abanguni yaani kwa kiswahili tunaweza kusema Wanguni. Kwa kipindi chote hiko kwenye ardhi ya kusini mwa Afrika wakazi wote walikuwa wakifahamika kwa jina moja la Wanguni isipokuwa wale Khoisani. Na kwa miaka yote hiyo walikuwa wakiishi sehemu moja tu na hakukuwa na uhamiaji wowote nje ya ardhi ya Wanguni. Lakini miaka ya 1550, kunaingia wageni kusini mwa Afrika yaani Wadachi. Na ilipofikia miaka ya 1600, kukaja wageni wengine ambao ni Waingereza. Na kutokana na maslai ya kiuchumi,kidini na kisiasa kulipekea wageni hao kupigana kitu kilichopelekea migogoro mikubwa kusini mwa Afrika.

Inasimuliwa kuwa, migogoro hiyo ilipelekea vita vya Mfekane miaka ya mwanzo ya 1800. Na vita hivyo vikasababisha baadhi ya koo za Kinguni zilizokuwa kwenye makundi makubwa kuhama na kuelekea Afrika mashariki na kati. Sasa wakati koo hizo zinatoka huko zilikuwa zikifahamika kama Wanguni. Lakini mambo yalikuja kubadirika kadri sehemu walizokuwa wanapita. Kwa mfano wakati Zwangendaba na Zwinde wanafika kwenye ardhi ya Wathonga, Wathonga waliwaita Wangoni. Wao walitoa “U” na kuweka “O” kulingana na sheria na utaratibu wa lughu yao. Na hapo ndipo mabadiliko yalivyoanza kutokea katika zile koo maarufu za Wangoni, kutoka Wanguni hadi kuwa Wangoni. Wangoni walifanikiwa kufika mpaka Malawi kwenye miaka ya 1840/1850, hapo Malawi kulikuwa na makabila mengi sana. Ila yaliokuwa yakifahamika ni Wayo ambao nao walikuwa wahamiaji waliokimbia adha ya biashara ya utumwa iliokuwa ikifanywa na Wamakua. Hivyo kwa Wayao, Wangoni waliitwa Wagwangwala wakiwa na maana ya watu wenye haraka, na hii ni kutokana na muonekano wa Wangoni kwenye ardhi ya Wayao. Mpaka kufikia kwenye miaka ya 1860, Wangoni walifika kwenye ardhi ya Wahehe, Wahehe walipigana na Wangoni na hivyo Wahehe waliwapa jina Wangoni na kuwaita Wamapoma au Wapoma wakiwa na maana ya Wavamizi walovamia ardhi ya Wahehe na kuanzisha mapigano kuanzia kwa Wabena pamoja na Wasangu.

Lakini mpaka kufikia miaka ya 1870, Wangoni waliweza kufika kwenye ardhi ya Unyamwezi na Usukuma ambapo huko waliitwa Watuta. Na kuna baadhi ya maeneo ya ziwa Tanganyika, Wangoni waliitwa Watuta pia kwa makabila kama Wafipa waliokuwa na ufalme wao kwa wakati huo. Kwa ujumla tukianza kuuliza kila kabila lililokuwa limefikiwa na wangoni, tunaweza kupata majina mengi sana kulingana na idadi ya makabila tulionayo. Kwa sababu ujinaishaji wa makabila yetu ulikuwa unategemea sana mitazamo aidha ya wazawa au wageni.

Tukimaanisha kuwa kuna makabila yamepata majina kutokana na wao wenyewe kujiita hivyo, na kuna wengine walipata majina kutokana na utani au mtazamo wa wageni. Hivyo tunaweza kuwaita Wangoni kwa majina mengi sana lakini uridhi wa makabila unategemea masimulizi ya wazee kutoka kizazi hadi kizazi.

Hivyo kama leo hii tunawafahamu Wangoni kama Wangoni,basi hayo ni matunda ya kuhifadhi urithi wa kabila hili. Kama si hivyo pengine wanahistoria wangewajua Wangoni kama Wagwangwala au Watuta. Hii ndio habari na historia nyingine ya kabila la Wangoni.Marafiki-wa-enzi.GIF

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, sijui una madigirii mangapi. Piga stori nyingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa… soma zaidi

a.gif Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka🐈,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wanakijiji wanahaha kusaka Paka🐈,
wanawaleta mchina ananunua wote anasepa
nao. Anarudi tena anasema vipi, naona
wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya
35,000 Paka🐈 mmoja, wanakijiji wanaenda
deep zaidi msituni, kamata Paka🐈, leta kwa
mchina, mchina anasepa nao… soma zaidi

a.gif Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako "Romantic". Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe… soma zaidi

[Kitendawili Kwako] 👉Mchana Wablue usiku Mweusi

[Chemsha Bongo Kwako] 👉Je hapa sisi tuna Macho Mangapi?

UJUMBE-POLE-NDUGU.JPG

a.gif Ndoa nyingine ngumu sana. Soma kisa hiki

Misingi mingine ya ndoa zetu ni migumu sana.
Pata simulizi hii toka Marekani… soma zaidi

a.gif Mapishi ya Mihogo ya nazi na kuku

Mihogo kilo 1
Kidali cha kuku 1 kikubwa
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu maji 1 cha wastani
Swaum/tangawizi i kijiko cha chai
Nazi kopo 1
curry powder 1 kijiko cha chai
Binzari manjano 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili 1
Chumvi kiasi.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2.. soma zaidi

a.gif Athari za Moshi wa sigara kwa mtoto

Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuwa watoto wazazi wao walivuta sigara mbele yao,wana hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na maradhi ya mapafu… soma zaidi

a.gif Ukubwa wa uume si kigezo cha kumridhisha mpenzi wako

Utajuaje kuwa ni kubwa au ndogo? Obviously ni kwa kujipima….lakini wanaume wengi wanapenda au hata kujisifia kuwa wao ni wakubwa, wakidhani ni moja ya sifa au hitaji la muhimu la wanawake… soma zaidi

[Msemo wa Leo] 👉Kutokuwa na kitu

[Jarida la Bure] 👉Jarida la kilimo bora cha HOHO

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

UJUMBE-HONGERA-NDUGUU.JPG
UJUMBE-MSAMAHA-35JHF32.JPG

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.