Historia ya asili ya neno Zanzibar

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Wewe ni mshindi, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Historia ya asili ya neno Zanzibar.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Historia ya asili ya neno Zanzibar

By, Melkisedeck Shine.

Zanzibar ni moja ya kisiwa kinacho patikana katika Pwani ya Afrika Mshariki. Ni miongoni mwa maeneo yenye historia ndefu sana barani Afrika. Tunaweza kuzungumzia mengi sana huu ya Zanziabr. Ila kwa leo tupate kufahamu habari za Jina Zanzibar.

Ukweli ni kwamba kila kilichopo hapa duniani kina historia yake. Na ifahamike kuwa kabla ya kuja kwa wageni katika bara la Afrika, kila kitu kIlikuwa na jina lake. Na majina mengi yaliyokuwepo na mengine bado yapo, yalikuwa na uhusiano wa karibu sana na jamii za kiafrika. Lakini mara baada ya ujio wa wageni kulikuwa na utajaji mpya wa baadhi ya maeneo (yaani kwa mitazamo yao) . Na hii ilisababishwa na wageni kuwa na taaluma ya uandishi ambapo waliweza kuandika habari za Waafrika kulingana na sera na mfumo wa maisha yao. Wageni tunawazungumzia hapa ni kuanzia Wagiriki mpaka Waarabu. Na zaidi ya hapo kulikuwa na maeneo ambayo yalipata majina mengi kwa wakati tofautitofauti kulingana na ujio wa wageni. Mfano mzuri ni kisiwa cha (Unguja) Zanzibar. Hapa inatupasa tuelewe kuwa tunachokiangalia hapa ni neno Zanzibar na habari za Unguja tutaangalia kwa upande mwingine. Inasimuliwa kuwa, wakazi wa kwanza kuishi kisiwa cha Zanzibar ni Wabantu, na kwa mujibu wa Prof. Chami aliyefanya tafiti zake Zanzibar alitoa ushahidi wa uwepo wa makabila ya kibantu katika maeneo hayo kabla ya wageni kufika miaka ya 600 BK/BM. Na hata Mwalimu Abdalah Bashiri nae anasisitiza hivyo.
Inasimuliwa kuwa, Kipindi hiko cha Wageni, Neno Zanzibar lilikuwa na maana ya eneo lote la Pwani linalopatikana kuanzia kusini mwa Somalia ( Mto Juba) hadi maeneo ya Msumbiji. Inasimuliwa kuwa, Kabla ya kuitwa Zanzibar, hapo mwanzoni kwa mujibu wa wageni, walipaita Zanji/Zenji/Zinji bila kuongeza “Bar”, wakiwa na maana ya Watu Weusi.lakini tukirudi nyuma, hasa kwenye vita vya kiislamu huko Uarabuni miaka ya 700, kulichukuliwa Waafrika zaidi ya 400 kutoka Pwani ya Zanji na walifahamika kwa jina la Wazanji*watu weusi*.
Kwa uchanganuzi tu neno Zanji kwa Kiswahili ni Zanchi yaani nchi ya Za. Ikiwa na maana ya Za- maeneo yote yaliyozunguukwa bahari ya Hindi. Na neno Chi au Nji lina maana ya ardhi. Kwa hapo tukapata maana ya watu weusi waliokuwa wakiishi kwenye ardhi (kisiwa) kilichozunguukwa na bahari ya Hindi. Na baadae kwenye miaka ya 1200/1300 Waarabu walitaka kutofautisha baadhi ya watu wakaongeza neno “Bar” ikiwa na maana ya ardhi inayomilikiw na wa Zanji. Na hivyo kupata Zanjibar au Zanjbar. Na hata ushahidi wa maandiko ya Ibn Hawqal yalionesha kuwa mji huo ulifahamika kama Zangbar kutokana na maandishi na matamshi yake. Na hata kwenye karne ya 12 sawa na miaka ya 1100 kwenye maandiko ya Al-Idris aliandika Zangbar ikiwa na maana ile ile. Na hata Wachina walipofika maeneo hayo waliyatambua kwa jina la (Ts’ong-pa) ikiwa na maana ya Zangbar. *Na mpaka Wareno walipofika maeneo hayo kama Vasco Da Gama na Marco Polo walitambua eneo kama Unguja. Hivyo neno Unguja lilikuja kufahamika mara baada ya ujio wa Wareno. Lakini bado walisikia na kuona watu wakipatamka kwa jina la Zanj Tukiachan na habari za Unguja, turudi kwenye suala zima la Zangbar. Historia inafafanua kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya uangalizi wa Mwingereza kuanzia miaka 1890, na hata wakati huo Wazungu walipatambua kama Zanzibar, ili kurahisisha matamshi ya kiingereza.
Zanzibar ilipata uhuru mwaka 1963 na uhuru huo ulikuwa wa wachache. Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1964 kulifanyika mapinduzi kisiwani hapo. Na mwaka huohuo mwezi wa 4, Zanzibar iliungana na Tanganyika na kuunda Tanzania. Mchakato ulikuwa hivi wa kuunda neno Tanzania.
Zilichuliwa herufi 3 za mwanzo kutoka kwenye kila neno, yaani Tan-kutoka Tanganyika na Zan –kutoka Zanzibar na kupata Tan+zan-. Na mwisho kuchua herufi zilizobakia yaani kutoka Zanzibar tukapata –a- na Tanganyika tukapata –i- na mwisho tukapata –ia- na kuzaa neno Tanzania,yaani Tan+Zan+ia Na hii ilifanywa na Hayati, Julius Kambarage Nyerere kutoka Tanzania na Hayati Shekhe Abeid Amani Karume kutoka Zanzibar . Ukweli ni kwamba licha ya changamto nyingi muungano huu una faida sana kwa nchi hizi.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Historia ya asili ya neno Zanzibar, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

UJUMBE-WA-MCHANA-KWA-NDUGU.JPG
MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG