HABARI NA HISTROIA YA KABILA LA WAGIRIAMA. Katika nchi ya Kenya kuna kabila linafahamika kwa jina la Wagiriama. Kiasilia kabila hili linatokea kwenye familia lugha ya Wakushitiki,ambao wanahistoria wengi wanakubaliana kuwa walitokea maeneoa ya Uhabeshi yapata miaka ya 1000.
Kabila hili nchini Kenya linapatikana kando kando ya mto Athi na pia kwa sasa wanapatikana maeneo mengi ya pwani ya Kenya ikijumuisha Mombasa mpaka Lamu.shughuri kubwa ya kabila hili ni ufugaji kama ilivyo kwa makabila yanayopakana nao kwa mfano Wamasai. Kama inavyofahamika kuwa, makabila mengi ya kiafrika yamekuwa na tamaduni nyingi sana ambazo wengi zimekuwa zikitushangaza kwa wakati huu wa sasa. Wengine tumekuwa tukijiuliza ni kwa namna gani watu Fulani waliweza kuanzisha tamaduni Fulani. Lakini jambo la msingi ni kwamba suala la uzuri na ubaya wa tamaduni Fulani unategemea kabila husika.
Na mara bada ya kufahamu haya machache, tupate kujua tamaduni za kabila la Wagiriama ambazo zinaweza kukustahajabisha. Nitajadili mambo kama, suala la ndo na suala la mazishi. Suala la ndoa, kwa wagiriama ni moja ya jambo muhimu sana na kila mwanajamii ndoto zake ni kuwa mume au mke wa mtu. Na mara baada ya kijana kufikisha umri wa kuoa kuna namna mbil za kupata mchumba. Njia ya kwanza ni ile ambayo kijana wenyewe anatafuta mchumba. Na njia ya pili ni ile ambayo wazazi ndio wanamtafutia mchumba kijana wao . Na kuna aina tatu za ndoa kwa kabla la wagiriama, moja ndoa ya kuchumbiana ambapo mvulana huenda nyumbani kwa msichana na kueleza dhima yake ya ndoa. Aina ya pili ni ndoa ya kumtorosha msichana kutoka kwao. Na aina ya tatu ni ndoa ya kumuiba msichana kutoka kwa mume wake na sio nyumbani kwao. Mfumo wa mahari huwa ni ngo’mbe na kama hakuna ng’ombe basi watatoa kondoo. Lakini thamani ya ng’ombe mmoja ni sawa na kondoo kumi. Siku ya mvulana kumtongoza msichana atatakiwa kwenda na rafiki yake, na msichana akishafahamishwa ujio wa mvulana huyo nyumbani hapo, basi msichana nae atatafuta rafiki yake. Na mwisho wa siku suala la kutoa maelezo yanafanywa na marafiki na sio walengwa. Siku ya kufunga ndoa kunafanyika mambo mengi sana, Kwa mfano wazazi wa pande zote mbili wataandaa chakula kwa kuchinjwa mifugo mbalimbali. Na mara baada ya ndoa kufungwa wakati wa mchana, watu watarazimika kuselebuka mpaka mida ya usiku ndipo bibi harausi na bwana harusi pamoja na majamaa wengine wataondoka. Kabla ya mida ya usiku, bibi harusi anapewa muda wa kuwaaga ndugu na jamaa zake na kisha kuchagua baadhi ya ndugu akiwemo shangazi, bibi na baadhi ya mama wadogo kwa lengo la kumsindikiza. Na huku nako bwana harusi alishakuja na ndugu na jamaa zake tayari kwa kuchukua mke wake. Na ifikapo mida ya usiku bwana harusi na bibi harusi watatakiwa kufunga safari kwenda nyumbani kwa bwana harusi. Sasa wakishafika huko, kwenye familia ya bwana harusi. Kwa mara ya kwanza kaka wakubwa wa bwana harusi watatiwa kulala na bibi harusi kabla ya mwenye mke kulala nae. Hii inamaanisha kuwa, kama kuna kaka 10, basi bwana harusi ana muda wa siku 10 akisuburi kaka zake wafanye mambo kwanza. Na kama kaka wapo 36, basi bwana harusi atanzaa kulala na mke wake mwezi ujao maana idadi ya kaka ni zaidi ya siku zilizopo kwenye mwezi mmoja. Sababu ya kufanya jambo hili, inadaiwa kuwa ni kumkaribisha bibi harusi kwenye familia yao. Na endapo itafahamika kuwa bibi harusi alikuwa bikra, basi kaka hao watarazimika kutoa zawadi nyingi sana isiokuwa na kipimo kwa bwana na bibi harusi na bwana harusi kuheshimika na familia pamoja na kijiji kizima. Kwa upande wa mazishi kuna mambo ya ajabu kidogo, kwani mazishi hutegemea mambo kama jinsia, umri na ulemavu. Tunaposema jinsia tunamaanisha mazishi ya mwanaume na mwanamke yalikuwa tofauti sana kwa wagiriama.
Na tunaposema umri tunamaanisha mazishi ya mtoto ni tofauti na mazishi ya kijana au hata mzee. Jambo la kushangaza hapa ni pale ambapo kama mtoto atazaliwa kwa kutanguliza miguu, atauawa na mazishi yake yanafanyika bila kumfunika sanda lakini kabla ya kufukiwa, kama ni mwanamke wanamuacha hivyo hivyo na kama alikuwa wakiume watamchanja kidogo kama ishara ya kuonyesha kuwa, endapo angekuwa mkubwa angetailiwa. Lakini pia hata kwa mtoto alikuwa ameota meno ya juu kabla ya chini pia atazikwa kwa mtindo huo Kwa wanajeshi, wenye ukoma na watoto wenye ulemavu walizikwa mbali na makazi ya watu kuepeusha laana na mikosi na hakukuwa na matanga kwa watu hao. Kwa wagonjwa hasa wa ukoma, baada ya kufariki, nyumba na vitu vyote vilivyokuwa vinatumika viotachomwa moto. Hizi ndio habari na historia ya kabilala Wagiriama. Habari na historia hii ni sehemu tu ya kabila la Wagiriama.


Slide3-mabestimliopotezana.PNG

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Historia na Habari ya Kabila la Wagiriama).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Makala nzuri kwa sasa👇

A

nn.gif