Eti jamaa mmoja akaja kwangu akawa anang'ang'ania kunisimulia matatizo ya familia yake.

NIKAMSTOPISHA nikamwambia " Unadhani
familia yako ina matatizo?" Nikaamua kumpa yakwangu.

"Miaka michache iliyopita nilikutana na
mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu,
mimi na huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye
baba yangu ambae alikuwa mkiwa baada ya
kufiwa na mama kitambo tu akaamua kumuoa
binti yangu wa kambo (yaani binti wa huyu mke
wangu niliyemwoa akiwa mjane), hivyo huyo binti
yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo
na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa
kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe
wa mkwe wake.
Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa
kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba
yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo)
alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume
akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia
baba mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto
wa binti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu
wa mke wangu na mimi nikawa babu yake huyo
mdogo wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na
mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa
msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia
ni mke wa baba yangu) ambaye ni ndugu wa
mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia
mama yao mmoja, akawa pia bibi yake na
mwanangu (mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba
yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu (achilia
kuwa babu yake!!) ambaye ndugu yake wa kike
kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba
yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama
yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama
mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto
wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu
ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
Kabla sijammalizia jamaa akaondoka


tafuta-rafiki.gif

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Haya ndiyo kweli matatizo).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Makala nzuri kwa sasaπŸ‘‡

A

uliyesoma.gif