HABARI NA HISTORIA NYINGINE YA WAZIGUA. Habari za Wazigua, Wasambara na Wabondei. Ifahamike kuwa katika bara la Afrika, makablia yaliyo mengi ni kutoka familia lugha ya Wabantu. Licha ya kwamba makabila hayo yanaishi mbalimbali na kwa mtindo tofautitofauti, ukweli ni kwamba makabila haya yanafanana sana. Kwa mfano kuna mfanano mkubwa sana kati ya kabila la Wadogoni kutoka Afrika magharibi na kabila la Wamakonde kutoka kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji.
Ukiachana na makabila hayo ambayo yapo mbalimbali, kuna makabila ambayo watu huzani kuwa wanatofautiana kumbe ukiyafuatilia kwa undani utagundua kuwa makabila hayo hayafanani. Ukweli ni kwamba japo makabila hayo yanatofautiana kwa kiasi fulani kutokana na mfumo wa maisha, lakini yanafanana sana. Mfano mzuri ni makabila ya Wazigua, Wabondei na Wasambara. Makabila haya yote yanapatikana kaskazini-mashariki mwa nchi ya Tanzania. Ni makabila yanayopatikana katika mikoa ya Tanga ( Handeni, Amani, Lushoto, Muheza) na Morogoro ( Tuliani).
Kwa mujibu wa East African literature Bereau, wanafafanua kuwa, Wasambara na Wabondei asili yao ni Wazigua. Inasemekana kuwa Wazigua walipofika hapa Tanzania wakitokea Kenya ( na inasemekana Kenya walipita), walikuwa wakifanya shughuri za ufugaji. Na inasemekana ni miongoni mwa kabila liliokuwa kubwa kwa miaka ile ya 1700/1800. Walikuwa wafugaji wakubwa wa ng’ombe.. Waliamini kuwa maisha yao yalikuwa yakitegemea sana ng’ombe.na Kuna kipindi kulitokea ugonjwa ambao uliua mifugo mingi bila kusahau vita vya Wenyewe kwa Wenyewe.
Kutokana na hali hiyo baadhi ya Wazigua waliamua kuondoka na kusambaa sehemu mbalimbali. Na ikumbukwe kuwa wakati Wazigua hao wakisambaa, walikutana na makabila mengine ambao waliwaita kwa majina mengine (haikufahamika ni makabila gani). Huko pia waliweza kuoana na kuzaa watoto wenye mchanganyiko wa damu. Mbali na ugonjwa wa ng’ombe, Wazigua walikuwa na tamaduni za kuua watoto waliokuwa wakizaliwa na magego na waliitwa kwa jina la Vigego. Kwa namna hiyo kulikuwa na watu ambao hawakupenda tamaduni hizo, hivyo waliamua kuondoka na kusambaa sehemu mbalimbali. Wakati Wazigua hao wanasambaa sehemu mbalimbali walikuwa wakiogopwa sana hasa kwenye ardhi ya Wadoe karibu na maeneo ya Pwani.
Kwani inasemekeana kuwa Wazigua walikuwa wakimiliki bunduki na zingine hatari za kijadi. Inasimuliwa kuwa Bunduki walizipata kutokana na biashara waliokuwa wakifanya na Waarabu kwa wakati huo(sio utumwa). Hivyo basi wale Wazigua waliokuwa wakisambaa ndio leo hii tunawaida Wasambaa. Na wale Wazigua waliokimbilia mabondeni ndio hao tuliokuja kuwajua kama Wabondei yaani waliokaa mabondeni.
Kwa ujumla Wasambara na Wabondei ni makabila yenye kugawanyika kutoka katika kabila la Uzigua. Na hata ukiangalia lugha zao zinafanana sana. Ukweli ni kwamba kabila la Wazigua na makabila mengine yalikuwa yakitawanyika sana. Na baadhi ya wataalamu wanaita jamii zenye kuhamahama. Na hii ndiyo sifa ya makabila mengi ya kibantu.

#morning


utotoni.gif

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Habari na historia ya Wazigua).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Makala nzuri kwa sasa👇

A

KUKUTANA-MPENZI-FG94T.JPG