Habari na historia ya Mkwawa kuvamia ardhi ya Ugogo

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Soma hapa wewe kijana wa kiume, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Habari na historia ya Mkwawa kuvamia ardhi ya Ugogo.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Habari na historia ya Mkwawa kuvamia ardhi ya Ugogo

By, Melkisedeck Shine.

Mkwawa alikuwa mmoja ya Kiongozi wa kabila la Wahehe, aliyepata kujiwekea historia kubwa sana katiba bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla. Alifanikiwa kurithgi uongozi kutoka kwa Mwinyigumba kutokana na ushupavu wake katika kujengwa na kuendelea ufalme wa Uhehe miaka yab 1800. Hivyo katika kuhakikisha anafanya upanuzi wa utawala wake, Mkwawa ailijaribu kuvamia ardhi ya Ugogo ambayokwa miaka ambayo anafanya uvamizi huko Ugogoni kuliluwa na jamii za Kigogo zilizopata kukua. Hivyo kwenye makala hii fupi utapata Kufahamu habari na historia ya Chifu Mkwawa kuvamia ardhi yaUgogo.

Kama ilivyofafanuliwa kwenye maandiko yenye kuhusu historia ya Afrika, hasa kwenye miaka ya 1700/1800, kuwa nchi/tawala nyingi zilikuwa na sera ya kupanua mipaka. Wakati huo heshima ya nchi au jamii fulani ilitegemea sana kuwa na uongozi imara na wenye nguvu wakati wote. Na kulikuwa na jamii au nchi zilizokua kwa sababu mbalimbali, kwa mfano zipo nchi zilizopata kukua kutokana na vita, zipo nchi zilizopata kukua kutokana na biashara na zingine zilikua kutokana na uhamiaji kwa mfano ule wa Wangoni kutoka kusini mwa Afrika.
Na ifahamike tu kwamba jamii za kizamani hazikuwa zinaridhika kutokana na ukubwa wa nchi hizo au mali walizonazo, kwani watu walikuwa wakiongezeka siku hadi siku. Na pia kulikuwa na mtindo wa kuhamia nchi moja kwa lengo la kupata usalama zaidi, ambao nao ulichangia kwa kiasi kikubwa kukuza nchi/tawala.
Na hii ilitokea sana kwenye jamii za kitanzania, kwani kuna baadhi ya jamii ziliamua kuungana kutokana na kuwepo kwa jamii zilikuwa zikipenda sana vita. Kwa mfano Wadoe waliamua kukimbia ardhi yao na kwenda Uzaramo kutokana na vita vya Wazigua. Na suala zima la vita kwa jamii za kizamani zilikuwa zikichochewa sana na kiongozi ambaye alionekana kuwa Shujaa kwa jamii hiyo. Kwa mfano kabila la Wahehe, ni miongoni mwa kabila ambalo lilipata kujiwekea heshima kubwa na historia kubwa katika ardhi ya Tanzania. Kwani Mkwawa alifanikiwa kupigana na jamii nyingi na kuziteka jamii hizo na zikawa chini chake. Ni moja ya kiongozi aliyefanikiwa kuvamia na kuteka jamii za Ugogo na kuzifanya zikawa chini yake, zikiwa huko huko kwenye ardhi ya Ugogo. Na hii ni tofauti kwa mashujaa wengine, kwani viongozi wengine walikuwa wakichukua mateka na kuwapeleka kwenye ardhi yao. Kwa mfano Mtemi Mirambo aliafanikiwa kuwateka Watusi, Wasukuma na Wanyaturu na kuwapeleka kwenye ardhi ya Unyamwezi. Ila kwa Mkwawa alifanikiwa kuziteka jamii za Ugogo na kuzitawala zikiwa kwenye ardhi ya Ugogo. Inafafanuliwa kuwa katika mwaka 1880, Mkwawa alifunga safari kwenda Ugogo hasa maeneo ya Nondo kwa lengo la kuweka utawala wa Kihehe huko Ugogoni.
Kipindi Mkwawa anapanga safari ya kwenda Ugogoni bado kwenye ardhi ya Uhehe, kulikuwa na ujio wa Wangoni waliokuwa wakifanya vita kila walipokuja. Mkwawa alijitahidi sana kupigana nao hasa kwenye miaka ya 1882 kwenye maeneo ya tamabarare ya Ulanga. Na mwisho wa siku Wangoni walipigwa na Wahehe. Na hapo ndipo Wangoni walipoamua kuungana na Wahehe, licha ya kwamba Mtemi Chambruma wa Wangoni alikataa kuunga mkono suala hilo. Hapo awali Mkwawa aliwaona Wangoni kama kikwazokwa yeye kufanya upanuzi kwa kuvamia Wagogo. Lakini baadae alikuja kuona faida ya vita kati yake na Wangoni. Kwani mara baada ya Wahehe kuungana na Wangoni, Wahehe wakawa na jeshi kubwa sana kiasi cha kufanikisha kuteka Ugogo na pia kuwapiga Wanyamwezi walioonekana kuvamia maeneo ya Igawiro. Hakika Wanyamwezi nao walionekana kuwa kikwazo kwa Mkwawa kuvamiaardhi ya Ugogo. Mapambano kati ya Wahehe na Wanyamwezi yalikuwa wakubwa sana. Lakini Kutokana na ukubwa wa jeshi la Mkwawa, Wanyamwezi walipigwa na kukimbizwa maeneo ya Ufipa na huko Unyamwezini. Na hapo ndipo Mkwawa alipofanikiwa kuteka na kuanzisha utawala wake katika nchi ya Ugogo. Na kipindi hiko hiko Mkwawa alifika mpaka maeneo ya Useke na wenyeji wa huo walikubali kujiweka chini yake na kuwa mtawala wa Useke. Na mara baada ya Mkwawa kutawala maeneo ya Useke, aliamua kushambulia jamii zilizokuwa zikiishi maeneo ya Kilosa , Wasagari na Vidunda na kufanikiwa kuanzisha utawala wake kule. Na hivi ndivyo Mkwawa alivyofanikiwa kutawala Ugogo. Japo hakufanikiwa kutawala maeneo yote ya Ugogo bado ilihesabika kuwa alipata kutawala huko. Kwa maana Mkwawa alifanikiwa kutawalaUgogo kwa upandewa kusini-Magharibi. Lakini kwa pande zingine ilikuwa vigumu sana hasa kwa Wamang’ati na makabilamengine kutoa Kaskazini-Mashariki(rejea makala ya Koo zilizounda kabila laWagogo).
Ukweli ni kwamba mpaka wakaoloni wanafika katika ardhi ya Ugogo, walikuta katika ardhi ya Ugogo kuna jamii zilizokuwa imara sana na zenye kujiamini sana. Na hii ni kutokana na kuwepo kwa Shujaa Mkwawa, ambaye alifanikiwa kuunda jeshi kubwa sana.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Habari na historia ya Mkwawa kuvamia ardhi ya Ugogo, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

FURSA.PNG

Fursa Ya Kazi Na Ajira Yenye Malipo Mazuri

Au soma zaidi hapa

.

NIMEKUMISI-MPENZI086H.JPG
UJUMBE-UNAVYOMMISI-NDUGU.JPG