HABARI NA HISTORIA YA MJI WA SINGIDA
Singida ni moja ya mkoa unaopatikana katika nchi ya Tanzania. Wakazi asilia wa mji huu ni Wanyaturu na Wanyiramba. Mji wa singida ni moja ya maeneo yenye historia kubwa sana ya nchini Tanzania. Wakazi wa mwanzo kabisa waliopata kuishi maeneo ya Singida, walikuwa ni Mbirikimo (Pygmies) waliopata kuishi hata kabla ya miaka ya 1000BK au BM. Lakini miaka ya baadae maeneo hayo yalikuja kuvamiwa na kukaliwa na jamii za kihamatiki ambao ndio hao Wanyiramba na Wanyaturu.
Baadhi ya wataalamu kama wakina mwalimu Bashir Abdalah waneleza kuwa “ wakazi hao asili yao Indonesia ambao walifika maeneo ya Afrika wakipitia baadhi ya sehemu mbalimbali barani Afrika na kufika hapo walipo leo.” Lakini pia hata kile kipindi cha ujuo wa kabila la Wamasai bado maeneo ya Singida yalikuwa moja ya maeneo ambayo yaliguswa na ujio wa Wamasai.
Inasimuliwa kuwa Wamasai pindi wanafika na kuvamia jamii za kaskazini yaani Wapare na Wachaga(Kwa kipindi hiko) walipigana vita kubwa sana. Wakati wanapigana vita kuna baadhi ya makabila kama Wandorobo na Wamang’ati waliamua kukimbilia maporini. Na maeneo hayo waliokimbilia miongoni mwao ni Singida.
kwani makabila hayo yalikimbilia Dodoma mpaka Tabora unyamwezini wakipitia hapo Singida. Na hata miaka ya baadae vita vilikuwa vimepamba moto baadhi ya Wamasai waliamua kukimbilia maporini. Na baadhi ya maeneo waliopita ni Singida. Mbali na hapo Singida ni moja ya maeneo ya mwanzo yaliopata kufikia na Waarabu waliofanikiwa kuanzisha biashara na kukuza dini ya Uislamu katika maeneo hayo kwenye miaka ya 700-1400. Lakini mpaka watu wa Ulaya wanafika maeneo ya Singida waliwakuta wenyeji hao wakiwa Waislamu kwa idadi kubwa.
Na hivyo wageni hao walianza harakati zao za kukuza Ukristo kwenye ardhi ya Singidan kama walivyofanya Waarabu kwa Kipindi hiko. Na hata mpaka kwenye miaka ya 1890, wakati Tanganyika inakuwa chini ya Wajerumani Singida ni moja ya maeneo yaliokuwa chini ya Wajerumani na kulijengwa makanisa na hospitali za misheni. Lakini pia kuanzia miaka ya 1920 Singida hasa maeneo ya Manyoni kulikuwa na uanzishwaji wa ofisi za kikoloni za Waingereza zilizokuwa zikisimamiwa na machifu pamoja na maakida.
Asili ya jina Singida lilikuwa na utata kwa kiasi fulanibkwani kuliibuka masimulizi mengi yaliotoa asili ya jina Singida. Na kama tujuavyo kuwa Waafrika hatukuwa na utamaduni wa kuhifadhi historia zao kwa njia ya maandishi. Lakini kwa kumrejelea mwalimu Abdalah Bashir anafafanua kuwa ‘asili ya jina Singida ni uwepo wa mitumbwi na kwa kikabila mitumbwi ni Singida. Na mitumbwi hiyo ilikuwa kwenye bwawa ambalo leo linajulikana kama Singidani.
Na hivyo wakati Wanyaturu wanafika maeneo hayo wakitokea maeneo ya kaskazini walisema wamefika “singidani” yaani kwenye mitumbwi. Na ndio maana mpaka leo mkoa huu unaitwa Singida na hata ukiwa pale Singida kuna bwawa linaitwa Singidani na kuna hotel nzuri ya KBH fika pale upate kufaidi upepo wa Singidani.


SALAMU-ASUBUHI-987HGZ.JPG

🙉🙉🙉Usisahau kushare posti hii kuhusu (Habari na historia ya mji wa Singida).👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome💯✔

Makala nzuri kwa sasa👇

A

PONGEZI-MPENZI-24498UA8.JPG