Habari na Historia ya Mji wa Pangani

By, Melkisedeck Shine.

Pangani ni moja ya wilaya inayopatikana katika mkoa wa Tanga. Wilaya hii inabeba historia ndefu sana kwenye nchi hii, Kwani Ni moja ya maeneo ya mwanzo kufikiwa na kukaliwa na Waarabu.Pangani ni miongoni mwa maeneo ya mwanzo ya Tanzania bara kufikiwa na wageni kuutoka mashariki ya kati miaka ya 600-900 ambao ndio hao Waarabu. Na hata kwenye miaka ya 1400, Pangani ni moja ya miji iliopata kufikiwa na Wareno.
Na hata vile vita kati ya Wareno na Waarabu Pangani vilifika na kuleta athari kubwa kwa jamii za mwazo za Wazigua.

Lakini hata kwa upande wa Wabantu wa mwanzo kufika maeneo ya Pangani walifahamika kwa jina moja la Waseuta( habari zake zilishasimuliwa kwenye habari za Wazigua).
Kihistoria kama inavyosimuliwa na wataalamu kama wakina Nkondokaya na wazee wa Tanga, wanasema kuwa mji wa Pangani ulianza kukua na kama unavyoonekana leo hii kuanzia miaka ya 1600/1700. Na mji huu ulipatwa kukuzwa na Wabantu ambao walikuwa wakifanya biashara na wageni kutoka mashariki ya mbali.

Na wakati mji huu unakuwa kulikuwa na maeneo ambayo yalipatwa kukaliwa na watu , maeneo hayo ni kama Hale, Maporomoko ya Muhembo na maeneo ya Mtindiro. Wanazidi kusisitiza kuwa mji huu wa Pangani wa sasa hivi ni mji wa sita kwani kabla ya hapo kulikuwa na miji mingine ambayo ilijengwa na kufa. Ukweli ni kwamba habari za mji wa Pangani zinajitoikeza hata kwenye vile vitabu vya masimulizi ya wasafiri kutoka Ugiriki( Periplus of Erythrean Sea). Na tunapozungumzia habari za masimulizi haya tunapata kusoma habari za mji wa zamani wa β€œRapta” uliopata kuwepo miaka ya 80(BK au BM)
Kwa upande wa machifu na viongozi mbalimbali waliopata kujenga historia ya mji wa Pangani, wanatajwa wakina Zume Seif, Zumbe Mwera,Zume Upanga na Wakina Zumbe Zuberi.

Asili ya jina hili Pangani linazua masimulizi mengi sana, hii inamaanisha kuwa kulizuka masimulizi mengi ambayo yalikuwa yanajaribu kusimulia asili ya jina Pangani. Kwa kumrejerea tena mwanahistoria Bwana Nkondokaya na masilimulizi niliyoyapata kutoka kwa watu wa Pangani, wanasema kuwa, asili ya jina Pangani linatokana na Pango au mapango yaliokuwa yakitumiwa na watu wa mwanzo kama makazi yao.
Aidha neno hili pangani ni la kibantu lenye maana ya pangoni kwani asilimia kubwa ya watu waliokuwa wakiishi kwenye mapango. Haikuishi hapo bado wanasema kuwa asili ya neno Pangani linahusiana na biashara ya utumwa. Kwani mji wa Pangani ni moja ya mji wenye historia kubwa ya biashara ya utumwa.

Wanasema kuwa neno Pangani linatokana na neni la kiswahili Pangani. Kwani watumwa walikuwa wakiletwa katika pwani ya Pangani, walikuwa wakipangwa kwa lengo la kusafirishwa kwenye majaazi. Na hivyo watu wakaamua kupaita Pangani kama jina la sehemu ambayo watu hupangwa kabla ya safari za majini
Kwa ujumla mji huu wa Pangani hasa kwa wakati huu ni moja ya sehemu za vivutio vya utalii nchini Tanzania. Kwani mji huu umehifadhi historia kubwa sana hapa nchini Tanzania tangu miaka ya 80 BK/BM mpaka leo hii.

Wilaya ya Pangani ina majengo mengi ya kale na yanatumika kama sehemu ya utaliiLeo hii pangani ni moya ya wilaya inayopatikana katika mkoa wa Tanga na wakazi wake wa asili ni wazigua hasa wale Waluvu, kutoka kwenye kundi la Waseuta. Hii ndio habari na historia fupi ya mji huu wa Pangani.

USIKOSE HIIπŸ‘‰ Biblia ya Kiswahili- Agano Jipya

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, sijui una madigirii mangapi. Piga stori nyingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa… soma zaidi

a.gif Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka🐈,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wanakijiji wanahaha kusaka Paka🐈,
wanawaleta mchina ananunua wote anasepa
nao. Anarudi tena anasema vipi, naona
wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya
35,000 Paka🐈 mmoja, wanakijiji wanaenda
deep zaidi msituni, kamata Paka🐈, leta kwa
mchina, mchina anasepa nao… soma zaidi

a.gif Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako "Romantic". Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe… soma zaidi

[Kitendawili Kwako] πŸ‘‰Hiki ni nini?

[Fumbo Kwako] πŸ‘‰Je, moshi ulielekea upande gani?

[Chemsha Bongo Kwako] πŸ‘‰Ni namba gani inayofuata hapa chini mwisho?

UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Fursa 150 za ujasiriamali, biashara na miradi nchini Tanzania

Zijue Fursa 150 za biashara na miiradi mbalimbali nchini
Tanzania… soma zaidi

a.gif Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?

Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuingia utu uzima,0 yaani kuwa mwanamke. Wasichana wanavunja ungo kati ya umri wa miaka 8 na umri wa miaka 18. Lakini, kuvunja ungo haina maana kwamba unahitaji kuanza kujamii ana. Kwa sababu ukijamii ana kuna hatari ya kupata mimba!.. soma zaidi

a.gif Mapishi mazuri ya Uji wa ulezi

Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula)
Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe)
Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai)
Siagi (butter kijiko 1 cha chakula)
Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili).. soma zaidi

a.gif Mambo ya msingi kwa mwanamke kuyajua unapojiremba

Kope nazo humpendezesha mwanamke kuna aina ya rangi za kupaka kwenye kope, lakini zinatofautiana. Ni vyema ukawasiliana na wataalamu wa mambo ya urembo kwa ushauri na siyo kukurupuka. Siyo umemuona fulani kapendeza na aina fulani ya rangi ya kwenye kope halafu na wewe ukakimbilia kupaka, utachekesha… soma zaidi

a.gif Mapishi ya choroko

Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima.. soma zaidi

[Msemo wa Leo] πŸ‘‰Uwezo wa Kutumia ulichonacho

[Jarida la Bure] πŸ‘‰Mapishi ya wali wa karoti na nyama

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.