HABARI NA HISTORIA YA MJI WA KOROGWE.

Korogwe ni moja ya wilaya inayopatikana mkoani Tanga nchini Tanzania. Mji huu kihistoria ni moja ya miji ambayo ilijiwekea historia kubwa sana. Hauwezi kuzungunzia habari au historia ya Wazigua bila kutaja mji huu wa Korogwe. Kama tulivyokwisha fafanua kwenye makala ya Wazigua na mgawanyiko wao. Na miongoni mwa Wazigua waliogawanyika, tuliwazungumzia Waluvu.
Waluvu ni moja ya kundi la wazigua waliotawanyika kutoka Ukilindi na kufika maeneo ya Luvu na kuitwa Waluvu yaani watu waliishi kandokando ya mto.Wazigua hawa ndio wenye kubeba asili ya neno Korogwe.
Hivyo Wazigua hao waliopata kuishi kwenye maeneo hayo na kufanya shughuri zao za kila siku. Walikuwa wakifanya shughuri za ufugaji na kilimo kwa kiasi kikubwa. Lakini miaka ile ambayo wageni kutoka mashariki ya kati na mashariki ya mbali wanafika maeneo hayo waliwakuta Wazigua wakiwa na maisha yao na wakiwa kwenye miji yao.
Wageni hao wanakadiriwa kufika kwenye miaka ya 1000, walifanikiwa kufanya biashara na kukuza dini ya kiislamu. Lakini pia haikuishia hapo, hata kwenye ile miaka ya 1400-1600 yaani ujio wa Wareno, Korogwe ulikuwa moja ya mji ambao uliwahi kufikiwa na wareno hao na walifanikiwa kuanzisha utawala wao na kukuza dini yao ya kikisto.
Lakini hata kwenye kile kipindi cha ukoloni hasa kile kipindi cha Ujerumani (1890-1920) na Waingereza (1920-1960) Korogwe ni moja ya maeneo ambayo yaliathirika sana na ukoloni. Kwani kihistoria mji wa Korogwe kama ilivyo kwa miji mingine ilikuwa na uongozi wake wa kichifu na uliokuwa ukishirikiana na sultani wa zanzibar. Hivyo ujio wa wakoloni kwa kipindi chote hiko kilikuwa na athari kwa Wazigua wa korogwe.
Na mara baada ya uhuru Tanzania ikatambua Tanga kuwa mkoa na kati ya wilaya 8 zilizopo mkoani Tanga, Korogwe ni moja wapo. Na ukiwa korogwe kuna miji mingi kwa mfano Mombo, Bungu na Magoma.
Kihistoria mji huu wa korogwe una asili yake, yaani asili ya jina korongwe linahusihwa na mtu. Inasimuliwa na wanahistoria mashuhuri kama wakina Nkondokaya na masimulizi ya Wazee kuwa, asili ya jina Korogwe linatokana na mzigua mmoja ambaye alifika maeneo ya Waluvu na kuanzisha shamba kubwa.
Mzigua huyo alifahamika kwa jina la Mnkologwe. Mzee huyo Mnkorogwe alikuwa maarufu sana kutokana na kumiliki shamba kubwa. Na inasimuliwa kuwa jina Korogwe ni la kiswahili ikiwa na maana kuwa, kulikuwa na utofauti wa kimatamshi miongoni mwa waswahili . Na hivyo wakajikuta wakitamka Korogwe badala ya Mnkorogwe.
Lakini pia kabla ya hapo Wazigua wenyewe walipaita Nkorogwe wakimaanisha eneo alilokuwa akiishi Mnkorogwe. Na mara baada ya mtu huyo kufa, kwa heshima ya mzee huyo na umaarufu wake wakaamua kupaita Nkorogwe na waswahili wakapaita Korogwe
. Unaambiwa kuwa, eneo ambalo ndilo lililobeba neno korogwe panaitwa Korogwe ya zamani na mji uliopo sasa hivi ndio korogwe mpya. Hakika mji huu una historia nzuri na yenye kuvutia sana. Hii ndio historia na habari ya mji wa Korongwe..


utotoni.gif

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Habari na historia ya mji wa Korogwe).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Makala nzuri kwa sasaπŸ‘‡

A

Slide3-mabestimliopotezana.PNG