Habari na historia ya Kijiji cha Ipole

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandalia makala inayopendwa kuhusu; Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali, sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

Habari na historia ya Kijiji cha Ipole.

Endelea kefurahia makala nzuri kila siku unapotembelea tovuti hii.

Habari na historia ya Kijiji cha Ipole

By, Melkisedeck Shine.

Ipole ni moja ya kijiji kinachoipatikana wilayani Sikonge, mkoani Tabora, takribani kilomita za umbali 22 kutoka wilayani Sikonge na kilomita 101 kutoka Tabora mjini. Ni moja ya kijiji ambacho kina kutanisha barabara ya kutoka Mbeya kuelekea Tabora, Shinyanga na Mwanza na pia barabaraya Rukwa kwenda Tabora, Shinyanga na Mwanza. Ukiwa kwenye kijiji hiki unaweza kuona safu za milima ya Ipole pamoja na misitu yenye kila aina ya miti.

Watu wa hapo asilimia kubwa ni wafanyabiashara, wafugaji pamoja na wakulima. Aina ya makazi ya hapo Ipole ni yale ya kukaa kando kando ya barabara yenye kuelekea maeneo tajwa hapo juu. Makabila ya sasa ni Wanyamwezi na Wasukuma. Kuna mengi ya kujua kuhusu kijiji hiki cha Ipole, mchache ni haya. Inasimuliwa kuwa, Ipole ya sasa hivi ilianza kwenye miaka ya 1970, na hivyo kulikuwa na Ipole ya zamani iliokuwa imeanzishwa kwenye miaka ya 1860. Hivyo kipindi Ipole ya sasa inaanzishwa kulikuwa na familia tano ambazo zilizopata kuwepo kwenye eneo hilo. Na familia hizo zilikuwa hapo kutokana na uwepo wa wamishioari. Hivyo kulikuwa na Ipole ya zamani kabla ya hii ya ipole ya sasa.
Wakazi wa kwanza kufika kwenye maeneo hayo ni Wanyanguru (Wanyanzaga) na Wagunda. Wanyanguru walikuwa wanatokea maeneo ya Mbeya wakati Wagunda walikuwa wanatokea upande wa Rukwa. Watu hawa walikuwa na vita pindi walipokuwa wanakutana kwa kuwa walikuwa wageni waliokuwa wanatafuta makazi na hivyo mapigano kila wakati. Inakadiriwa makabila haya yalifika hapo kwenye miaka ya 1860.
Asili ya jina hili Ipole linahusiana sana na lugha ya kinyamwezi. Inasimuliwa kuwa hapo mwanzoni kabisa kulikuwa na sehemu yenye chemchemu yenye maji ya baridi sana kutokana na aina ya miamba inayopatikana maeneo hayo.
Ndipo wakazi wa mwanzo kabisa waliotajwa hapo juu walikuwa wanaenda kuchota maji hapo. Na ndipo waliposema “minzi mapole” wakiwa na maana kuwa “maji ya baridi” na hivyo ndivyo palipojulikana kwa jina la minzi mapole na mpaka sasa kuitwa Ipole kutokana na makosa ya wafanya biashara na wamishionari walikuwa wanafika maeneo hayo. Kwa mujibu wa mzee Robert Uledi. Lakini pia ukiwa hapo Ipole unaweza kufahamu historia ya wamishionari waliopata kujenga makazi yao hapo na kujenga kanisa kwenye miaka 1903. Ukiwa hapo unaweza kuona mabaki ya majengo manne yaliokuwepo hapo kipindi cha ukoloni.
Mmishionari maarufu aliyewahi kukaa hapo ni Dr. David Livingstone aliyeweka kambi hapo akitokea Ulyankuru kwa mfalme Milambo, na kupitia maeneo kama Tutuo, Chabutwa na kufika hapo Ipole kabla ya kwenda kitunda. Kwa kipindi chote hiko alikuwa akitembea na mbeba mizigo wake, ambaye baadae alikuja kuwa mchungaji wa kwanza wa kinyamwezi Mch. Kipamila wa kanisa la Moravian miaka ya 1900. Lakini pia ukiwa hapo ipole unaweza kuona kaburi la aliyekuwa balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Uingereza miaka ya 1963. Alifahamikwa kwa jina la Christopher Kasanga Tumbo. Alizaliwa mnamo mwaka 1934 na kufariki mnamo mwaka 2002. Habari na historia ya mtu huyu zinajitegemea hivyo makala yake ipo. Kwa upande mwengine, historia inafafanuliwa kuwa kipindi cha kudai uhuru(1954) maeneo kama Chabutwa na Ipole ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaharakati wa TANU wakiongozwa na mzee Said Juma Nkumba. Lakini pia kwenye miaka ya 1960-1970 ,
kwenye ule mpango wa vijiji vya Ujamaa, kijiji cha Ipole ni moaja ya kijiji kilichokuzwa kwa kipindi hiko. Kwani inasimuliwa kuwa miaka hiyo ya 1970, kulikuwa na vijiji ambavyo vilivunjwa na kuunganishwa kwenye kijiji cha ipole. Vijiji hivyo ni kama Kininga, Msubha,Donga,Iwensato,Namkola Na Lukula. Wakati huo kiongozi wa kijiji alikuwa mzee Robert Uledi. Na hata kwenye vita vya Kagera vya miaka ya 1979, wakazi wa kijiji cha Ipole walijitolea vyakula na mifugo kwa wanajeshi wa Tanzania.
Leo hii Ipole ni moja ya sehemu ambayo inakua siku baada ya siku, kwani ukiwa hapo Ipole kuna huduma zote za kijamii na hivyo kuwavutia watu wengi sana.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; Habari na historia ya Kijiji cha Ipole, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

mtu.gif
Marafiki-wa-enzi.GIF