HABARI NA HISTORIA YA JIWE LA KUPIMIA WATUMWA.
Hakika historia ya biashara ya utumwa ina mambo mengi sana. kwa maana tangu tumeanza kusikia na kusoma habari za biashara ya utumwa , tumesoma na kusikia mengi sana. Wengine wanasema biashara ya utumwa Iinahusiana na dini, wengine wanasema biashara ya utumwa inahusu maendeleo ya biashara na wengine wanadai biashara ya utumwa ni mfumo tu wa maisha ya watu kama mifumo mingine. Wengine wanaenda mbali kwa kusema kuwa, historia ya utumwa sio sehemu ya maisha wala historia ya Waafrika, wakidai kuwa utumwa kwa Waafrika uliletwa tu na wageni. Wengine wanasema kuwa biashara ya utumwa ni sehemu ya maisha na historia ya Waafrika, kwa sababu biashara ya utumwa ilifanyika barani Afrika na kulikuwepo na baadhi ya Waafrika walihusika na walifaidika na biashara hiyo. Lakini kutokana na sababu za kimungu, kisiasa na kiutu, biashara hii ya utumwa ilikomeshwa. Japo kwa mtazamo wangu naona biashara hiyo haikukomeshwa bali ilipunguzwa makali. Au tunaweza kusema kuwa biashara ile ilitolewa kutoka kwenye uhalali kuja kusipo na uhalali. Lakini kwa namna Fulani hivi hali imebadilika kwani mambo si sawa na miaka ile ya 1400-1900. Hata kama biashara bado ilikuwepo lakini si sawa na ya miaka ile. Kwa ujumla kuna mambo mengi sana ya kuzungumza katika biashara ya utumwa. Kwa leo tutapata kufahamu kwa uchache habari na historia za jiwe la chuma lililokuwa likitumika kuthaminishia watumwa kabla ya kwenda kwenye sokoni. Jiwe hili linapatikana mkoani Mtwara, maeneo ya Mikindani nje kidogo ya manispaa ya Mtwara katika jumba lenye kuhifadhi historia na wakati huo huo ni hotel inayofahamika kama Old Boma. Inasimuliwa kuwa jiwe ilo lina uzito usiopungua kilo 30, Yenye umbo la duara kama linavyoonekana kwenye picha. Inasimuliwa kuwa jiwe hili lilikuwa linatumika kama sehemu ya kuthaminishia(kupima) watumwa kabla ya kwenda katika soko kuu la watumwa Zanzibar. Mambo yalikuwa kama ifuatavyo.
Kwanza, mara baada ya watumwa kukamatwa kutoka sehemu mbalimbali walifikishwa Pwani ya Mtwara Mikindani, ambapo kwa miaka ya 1800 ndio sehemu iliokuwa imeendelea sana, kwa na majumbwa ya kifahari. Wakishafikishwa hapo, watumwa walipaswa kupimwa na kuthaminishwa kama bidhaa. Hivyo mtumwa alipaswa kushika na kulinyanyua jiwe hilo la chuma kama sehemu ya kumthaminisha kama ana nguvu au lah!. Na akishafanikiwa kulinyanyua mtumwa huyo aliweza kufahamika na wafanya biashara kuwa ana nguvu kiasi gani na hata bei itapangwa kulingana na nguvu zake huku wakiangalia na muonekano. Na ikitokea mtumwa akashindwa kunyanyua jiwe hilo la chuma, mambo mitatu yalimtokea, moja aliachiwa huru aende zake kwa maana huyo ni dhaifu na afai kuwa bidhaa yenye ushindani. Lakini kuachiwa huru ilikuwa nadra sana. Pili aliuwawa kwa kuwa alikuwa mzigo usio na faida kwa mfanyabiashara, kwani angeweza kugharamiwa kwenye usafiri wakatisi bidhaa yenye thamani . Na mwisho alichukuliwa kama sehemu ya chambo hasa wakati wa kuvuka bahari ya Hindi. Mambo yalikuwa hivi, endapo wakatokea samaki wakali kama Papa na samaki wengine wakati wa kuvuka , ilirazimika kutupa baadhi ya watumwa ili kupoza njaa kwa wanyama hao. Kwa namna hiyo watu wengi waliokuwa wakisikia habari hizi waliogopa Sana. Na hata wale waliokuwa wamechukuliwa na ndugu zao waliwashawishi na kuwaomba kuwa wasishindwe kunyanyua jiwe lile kwani kuna mabalaa mengi sana endapo mtu akishindwa kunyanyua.
Kama nilivyosema hapo awali kuwa jiwe hili kwa sasa limehifahdiwa maeneo ya Mikindani kwenye Hotel na jumba la Historia Old Boma. Ili kujifunza mengi juu ya biashara ya utumwa fika pale na ujionee jiwe hilo lenye habari na historia ya kusisimua. Hii ndio habari na historia ya jiwe la chuma lililokuwa linatumika kuthaminishia watumwa.

#Morning brazaz n cstaz


NIMEKUMISI-MPENZI086H.JPG

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii kuhusu (Habari na historia ya jiwe la kupima watumwa).πŸ‘ Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasomeπŸ’―βœ”

Makala nzuri kwa sasaπŸ‘‡

A

tafuta-ndugu.gif