Kichekesho%20Kipya Usikose ๐Ÿ“•Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga๐ŸŒฟ๐Ÿ… Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10๐Ÿ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

ss.gif Fundisho : Usiwe unakurupukaโœ…

๐Ÿ‘Baada ya kusoma kuhusu๐Ÿ‘‡;

images-7.jpeg
๐Ÿ’กLeo nimekutayarishia๐Ÿ’ซ makala kuhusu๐ŸŒ  Fundisho : Usiwe unakurupuka๐Ÿ‘‡.

๐Ÿ’ฅFundisho : Usiwe unakurupuka๐Ÿ‘‡

Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguoza kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.

Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.

Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: โ€œ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?โ€

Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: โ€œ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitaliniโ€ฆ.. Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yanguโ€ โ€œPunguza hasira?!

Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?โ€ Yule Baba aliongea kwa hasira sana.

Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: โ€œDaktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Munguโ€

โ€œKutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sanaโ€ Alinongโ€™ona yule Baba mwenye mtoto.

Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, โ€œAsante Mungu! Mtoto wako amepona!โ€ Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!โ€ Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.

โ€œ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwananguโ€ Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.

Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:
โ€œMtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.โ€

HEKIMA:
1. โ€œUSIMHUKUMU MTU YEYOTEโ€ฆ. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI
KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.

2. โ€œTENDA WEMA KADRI UWEZAVYO BILAYA KUJALI HALI ULIYONAYO.
.
COMMENTT TRUE kama imekugusa kisha SHARE na wenzako waone.

๐Ÿ‘ŠUsikubali kupitwa na ๐Ÿ“•Kitabu cha Mbinu za Kilimo Bora Cha Mboga๐ŸŒฟ๐Ÿ…. Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10. ๐Ÿ‘‰Bofya hapa Kuchukua๐Ÿ‘ˆ

images-10.jpeg

๐Ÿ“Nini Maoni๐Ÿ’ญ yako Kuhusu Fundisho : Usiwe unakurupuka? Niandikie hapa๐Ÿ‘‡

Add a New Comment
or Sign in as Wikidot user
(will not be published)
- +
ACKYSHINE.jpg

๐Ÿผ Endelea kusoma kuhusu;-๐Ÿ™‰

.

.

.

.

.

๐Ÿ“ Misemo ya AckySHINE๐Ÿ‘‡

MA.gif
Kichekesho%20Kipya Usikose Jarida la Kilimo Bora cha Hoho Kilimo cha hoho kimeelezewa ๐Ÿ‘‰Bofya hapa KuchukuaKizuri

.

.

IMG_20170703_130405.jpg

Habari msomaji wangu…?
Jina langu ni Melkisedeck Leon Shine Mwendeshaji wa blog hii.

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa

Jina
Mahali ulipo
Mfano Mkoa, Wilaya n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako

KUHUSU BLOG HII | MAWASILIANO | ABOUT AUTHOR | LEGAL GUIDELINES