Badilisha fikra zako

By, Melkisedeck Shine.

BADILISHA MAWAZO YAKO HARAKA HUU NI MWAKA MPYA USIISHI KWA MAZOEA………..

Lazima miongoni mwetu tutakua kati ya hawa.

Hujawahi fikiria kama biashara ya maandazi ina hela sana hadi ulivyoona Baresa anauza,

Unakunywa bia kila mwezi lakini huna plan ya kufanya savings,

Umeshahudhuria mara nyingi sana vikao vya harusi na kuchangia lakini hujawahi hudhuria seminar za ujasiliamali,

Unatumia smart phone lakini kila siku unalalamika huna hela ya mtaji,

Unajua kumbi gani za starehe zinajaza sana lakini hujui ni biashara ipi unaweza ifanya kulingana na uwezo wako,

Kila Ukiwa social networks unajihusisha Sana na mambo yasiyo na manufaa ya kifedha kuliko yenye manufaa ya kifedha . ,

Kwako ni rahisi sana kusambaza msg kama vile za Anna Kansiime na Mkude Simba kuliko kama hii,

Tangu unapata mshahara wa laki tatu hadi sasa wa milioni mbili bado mshahara haukutoshi,

Unajua Beyonce katoa album gani, ana date na nani, anavaa nguo za nembo gani lakini hujui watu wanapataje hela kwenye masoko ya hisa,

Kila siku unaweza ukipata hela "isiyo na kazi" utanunua smartphone toleo jipya badala ya kuifanyia shughuli za kukuongezea kipato,

Kwako ni rahisi kukopa hela ya kumpa rafiki yake na shemeji yako kuliko kukopa hela na kufanya biashara ndogo.. ,

Biashara akiifanya mtu mwingine ni rahisi kuliko ukifanya wewe,

kwako ni rahisi kumuamini mtu anaekwambia 'ukitaka kuwa tajiri mtegemee Mungu' kuliko yule anaekwambia 'its not in God's plan to make you rich!',

Ukiwa unaangalia taarifa ya habari, unaishia za kitaifa tu au na za kimataifa, habari za kibiashara hazina
umuhimu kwako,

Uko radhi kutoka Mbagala Chalambe hadi Tegeta kumsalimia mpenzi wako lakini Chalambe hadi Ubungo kwenye seminar ya ujasilamali ni mbali sana kwako,

Unajua Diamond anaendesha gari la bei gani, Gwajima analipwa kiasi gani, msanii gani kafilisika, movie ya Ray ya mwisho iliingiza kiasi gani lakini hujui matumizi yako kwa mwezi ni kiasi gani,

Mtu akikuletea kadi ya mchango wa harusi ni rahisi kuchangia kuliko anaeleta mchango wa ada,

Kwenye whasapp groups unachangia sana maswala ya skendo, utani, fumanizi, mahaba, kejeli na kutumia muda mwingi sana kusoma au kuangalia mambo hayo kuliko mambo ya kutafuta hela, (Infact msg kama hizi zinakukera sana sababu kwanza hazikuchekeshi halafu ni ndefu!), vitu kama fursa za kibiashara, ujasiliamali, mchanganuo wa kibiashara hua unavisikia tu, hujawahi kuvitafuta au kufanyia kazi,. .

Kile kikao chenu cha kuanzisha kikundi cha kuweka na kukopeshana hela mlichopanga tangu mwaka jana hakijatokea lakini vikao vyote vya kukutana bar vimetokea, vingine bila hata kupangwa!!..

Mtu akikualika kwenye kufanya biashara unaona anataka kukutapeli, lakini anaekualika kwenye kula bata ndo wa ukweli….

TAFAKARI CHUKUA HATUAUJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG

Endelea kusoma makala hizi zifuatazo;

a.gif Ugonjwa wa kichomi

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.
Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.
Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa… soma zaidi

a.gif MAANA YA MAPENZI

Mapenzi Ni Hisia Kali Za Upendo Ambazo Humfanya Mtu Kujisikia Furaha Na Amani Ktk Moyo Wake. Vilevile Mapenzi Yapo Ktk Matabaka Mawili, Tabaka La Kwanza Ni Mapenzi Ya Yanayohusisha Jinsia Mbili Tofauti Au Moja Kwa Dhamira Ya Kuridhishana Kingono. Tabaka La Pili Ni Mapenzi Yanayohusisha Jinsia Mbili Tofauti Au Jinsia Moja Kwa Dhamira Ya Urafiki Na Sio Kingono… soma zaidi

a.gif Wakubwa nisaidieni!!

👉 Sio kila EX ni EXPIRED, EX zingine ni EXAMPLE:
Utanielewa tu.
Ulimwengu huu tunaoishi Muogope sana Mpenzi
wa Zamani wa Mkeo kabla HUJAMUOA na
Muogope sana EX wa Mmeo kabla HAJAKUOA
kuliko hata hawa Vidume na Vijike vinavyomtaka
akiwa tayari amevaa pete… soma zaidi

[Kitendawili Kwako] 👉Bibi anakung'uta matandiko

ndugu.gif

a.gif NJIA ZA KUONDOA KITAMBI

Mlo mzuri kiafya ndio ufunguo wa kupunguza uzito na kutoa kitambi. Kuacha kula vyakula vinavyotia nguvu sana, vyenye mafuta na sukari nyingi ndio msingi wa kuondoa kitambi. Hii husaidia mwili kutumia mafuta yaliyo mwilini kutengeneza nguvu hivyo kupunguza mafuta na kuondoa kitambi. Aidha, punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari kwa wingi na tumia samaki badala ya nyama… soma zaidi

a.gif SHAIRI: Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani… soma zaidi

a.gif Je, mtu anawezaje kuacha kutumia dawa za kulevya na itamchukua muda gani kurudia hali yake ya kawaida?

Kitu muhimu ni kwamba, kweli uwe umedhamiria kuacha. Hatua ya kwanza ni kujiuliza kwa nini unatumia dawa za kulevya. Pale utakapojua ni nini ulikuwa unahitaji katika dawa za kulevya ni rahisi kutimiza malengo hayo kwa njia za kiafya zaidi. Jaribu kupunguza taratibu kiasi na muda wa kutumia dawa za kulevya. Pia tumia vitamini na madini kuimarisha afya yako. Jitenge na watumiaji wengine wa dawa za kulevya na sehemu ulizokuwa ukienda kupata dawa za kulevya. Kama hutofanikiwa katika hatua ya kwanza usikate tamaa! Watu hushindwa kuacha katika jaribio la kwanza! Jaribu tena!.. soma zaidi

a.gif Je, ni kweli kwamba kuvuta bangi kunaongeza akili na uwezo wa kufikiri?

Hapana, hii si kweli! Vijana wanaoamini kwamba wana uwezo wa kufikiri baada ya kuvuta bangi kwa sababu inawapa hisia ya kuzoea mihemko ya kusikia vizuri au kufahamu kwa haraka. Lakini ni kawaida kwamba uvutaji wa bangi unaathiri shule, kazi na shughuli nyingine kinyume na matarajio ya mafanikio. Siku zote vijana wavutaji bangi wanapoteza ari shuleni au mafunzoni. Wanashindwa kuweka malengo ya maisha yao ya baadaye… soma zaidi

a.gif Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi i kukuambukiza virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa mii li yao. Virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye mii li yao, kwa sababu siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha na kuzaliana katika chembechembe nyeupe za damu, lakini chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu. Kwa hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza damu na aking‘ata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya kuambukizwa.
Thibitisho jingine la ukweli huu ni kwamba sisi sote tungekuwa tumebeba virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa anaambukiza kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira yenye mbu na karibu na watu wengine… soma zaidi

[Msemo wa Leo] 👉Ushauri kwa mtu

[Jarida la Bure] 👉DONDOO KUHUSU TEZI DUME

[Hadithi Nzuri] 👉Kisa cha kusisimua cha mama mjane

FURSA..! Kuna nafasi za kazi 100.

Au soma zaidi hapa

.

UJUMBE-WA-MSAMAHA-KWA-NDUGU.JPG
ndugu.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.