Jinsia ya mtoto angali mimba

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kike. Ile mbegu inayofika kwenye yai kwanza, inarutubisha yai na ni wakati uleule, jinsia ya mtoto i inatokea. Uwezekano wa kumpata mtoto wa kike au wa kiume unafanana, na hii ni kweli katika nchi zote duniani.

Je, unaweza kupanga kuzaa aina ya watoto, yaani wa kiume au wa kike tu?

Mimba i inatungwa wakati yai la kike linaporutubishwa na mbegu za kiume. Kama tulivyoona hapo juu, jinsia ya mtoto i inategemea aina ya mbegu za kiume. Nusu ya mbegu za mwanaume zinatengeneza mtoto wa kiume na nusu ya mbegu zinatengeneza mtoto wa kike. Lakini wanaume hawana uwezo wa kuamua aina ya mbegu i itakayorutubisha yai. Kwa hiyo, haiwezekani kupanga. Jinsia ya mtoto i nategemeana na bahati tu.

Je, kama mwanamke na mwanaume wanapata watoto wa jinsia moja tu, ni kosa la nani?

Hakuna mwenye kosa, kwa sababu jinsia ya mtoto i inategemea na bahati na hamna uwezekano wa kupanga kuzaa aina fulani ya mtoto. Tulivyoona juu ni mwanaume ndiye aliye na aina mbili za mbegu. Aina moja husababisha kutokea mtoto wa kike na aina nyingine mtoto wa kiume. Mwanaume hana uwezo wa kuhakikisha achangie aina ya mbegu gani. Kwa hiyo, hata kama ni mwanaume anayeyakinisha jinsia ya mtoto, hana kosa, kwa sababu hana uwezo wa kuamua achangie mbegu ya aina gani.