Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili

By, Melkisedeck Shine.

​1. Huwezi kubadili namna watu walivyokutendea mpaka ubadili namna unavyowatendea.​

Matayo 7:12;
"Basi yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii."

​2. Huwezi kubadili tabia mpaka ubadili marafiki.​

1Wakorintho 15:33
"Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema."

​3. Huwezi kubadili ulichovuna mpaka ubadili ulichokipanda.​

Wagalatia 6:7;
"Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."

​4. Huwezi kubadili mwelekeo wa maisha yako mpaka ubadili dereva.​

Kutoka 23:1-3;
"Msivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. Usiwafuate walio wengi katika kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotosha hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake".

Maisha yako yaweza ongozwa na mkumbo wa watu au ​MSIMAMO​ wako ​BINAFSI​ kwa ​UNACHOKIAMINI.​

​5. Huwezi kubadili hali yako ya kifedha mpaka ubadili tabia yako ya kifedha.​

Mithali 21:17;
Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; yeyote apendaye mvinyo, kula na manukato hatakuwa tajiri."

​Mtindo wa maisha ya ufukara ndiyo busara kwa wengi.​

​6. Huwezi kunibadili mpaka ujibadili mwenyewe.​

Matayo 7:3-5.
"Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako."

​7. Huwezi kubadili mtazamo wako wa kifikra mpaka ubadilipo usikiacho.​

Mithali 23:7;
"Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia haya kula, kunywa; lakini moyo wake hauwi pamoja nawe."

​(Waache wenye Hekima wasikilize na kuongeza ufahamu wao.)​

Huyo anayesikiliza, huashiria na kuamua kile anachojifunza.

Kile unachojifunza, huashiria uelewa ulio nao kichwani mwako.

Uelewa ulionao kichwani mwako, huashiria maamuzi yako.

Na maamuzi yako, huashiria ​mwelekeo wa maisha yako.​


Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili

a.gif Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu… soma zaidi

a.gif Kila kitu ni mali ya Mungu isipokua hiki

Kila kitu ni mali ya Mungu. Kuwa na Mungu ni kuwa na kila kitu. Hata mimi mwenyewe ni mali ya Mungu. Kitu kimoja tu nina hakika nacho kwamba ni mali yangu binafsi nacho ni dhambi zangu😛. Ee Mungu naomba niziungame niweze kubaki mali yako bila kuwa na kitu binafsi... soma zaidi

a.gif Nyimbo za Kwaresma za Katoliki

Hizi hapa nyimbo nzuri za Kwaresima zitakazokusaidia uwe na Kwaresima nzuri ya Tafakari.. soma zaidi

KADI-MMISI-MZAZI.JPG

a.gif Amri ya Sita ya Kanisa Inadai nini?

Inadai kushika Sheria Takatifu Za ndoa.. soma zaidi

a.gif Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?

Hapana, Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Ibada

Soma maswali haya ili kujua kuhusu ibada.. soma zaidi

a.gif Ni nini maana ya kuabudu sanamu?

Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake… soma zaidi

a.gif Nani huadhimisha Liturujia?

Liturujia iliyo kazi ya Kristo Kuhani Mkuu na kichwa cha Kanisa huadhimishwa na kusanyiko lote, kila mmoja kulingana na kazi yake… soma zaidi

a.gif Kampeni ya Kudumisha Umoja Wa Imani na Amani kwa watu wote

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Tarehe 15/05/2012 na Melkisedeck Leon Shine.
Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Umoja bila kuangalia tofauti za imani zetu za kidini… soma zaidi

a.gif Tafakari ya Zaburi 127:1-2

Leo tunatafakari Zaburi ya 127:1-2 kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria? Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.. soma zaidi

a.gif Nini maana ya Roho Mtakatifu?

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26).. soma zaidi

a.gif Kujinyima ni nini?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.