Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

By, Melkisedeck Shine.

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu.

Sumaki hii imewanasa hata ambao hawakutegemewa wala kutarajiwa.

Uzinzi uzinzi uzinzi umekuwa kama perfume ya kujipulizia kila Mara mtu akipenda.

Uasherati umekuwa kama heshima ya kibinadamu kwa vijana wengi.

Mbingu zimenyamaza kwa sababu iko jehanamu inawangoja wazinzi na waasherati.

Dhambi hii imekuwa sumaku kubwa ya shetani ya kukamata wanadamu ili waende jehanamu.

Wanadamu wa Leo ukimwambia kwamba aache uzinifu maana wazinzi na waasherati hawataenda uzima wa milele, mtu huyo anakuambia unamhukumu.

Ni Neno la MUNGU ndile limesema katika maandiko mengi tu kwamba wazinzi na waasherati sehemu yako itakuwa katika ziwa la moto.

Hata makanisani baadhi ya watu wamenasa kwenye sumaku hii.

Dada mmoja ambaye kila wiki anasimama na kushika mic kanisani kwao siku moja aliniambia kwamba hawezi kumaliza wiki bila kufanya ngono, na hajaolewa. Niliumia sana rohoni nikamwambia aache kutumika madhabahuni, yeye akasema itakuaje maana yeye ndiye tegemeo.

Mama mmoja alisema yeye ana mume mema sana na mume wake ni mwaminifu sana katika ndoa yao lakini yeye huyo mama ndio hutoka nje ya ndoa Mara kwa Mara, ni hatari inayohitaji neema ya MUNGU tu ili kutubu na kuacha.

Mama mmoja yeye ana watoto zaidi ya wawili na yuko katika ndoa lakini hana uhakika kama watoto wale ni wa mume wake wa ndoa, ni hatari sana.

Baba mmoja akiwa ndani ya ndoa amezaa watoto zaidi ya watatu nje ya ndoa tena wanawake zaidi ya wanne(4) tofauti tofauti.

Mwanaume moja ambaye husimama madhabahuni yeye kila Mara humdanganya mkewe kwamba anaenda safari kumbe ana mahawara karibia kila mkoa, ni hatari sana.

Watu wengi sasa wanaona uzinzi na uasherati ndio fashion nzuri ya wakati kuu.

Kila kijana ana girlfriend kwa lengo la ngono tu na sio vinginevyo.

Kila binti ana boyfriend kwa ajili ya uasherati.

Ukitaka watu wakuchukie basi kemea uzinzi na uasherati.

Watu wengi wamekuwa vipofu wa kiroho kwa sababu ya uzinzi na uasherati.

Lakini upo mwisho mmoja kwa watenda dhambi wote ambayo ni jehanamu.

Ndugu unahitaji kutubu Leo na kuacha dhambi.

Ndugu mmoja akasema yeye anaishi maisha matakatifu ila dhambi moja tu yaani uzinifu ndio imemshinda, hiyo ni hatari.

Leo hata ndoa takatifu zimeadimika maana wahusika huanza kwanza uzinzi na uasherati ndio baadae ndoa, ndugu mnahitaji kutubu.

Ndugu yangu unayenisikiliza kwa njia ya ujumbe huu nakuomba tubu na acha dhambi hiyo.

Amua kuiacha.

Mwisho wa uzinzi na uasherati ni kifo(Mauti) na baada ya kifo ni hukumu(Waebrania 10:27)

Nimekuonya wewe Leo ili ukishupasa shingo usije ukalaumu siku ile ukiwa katikati ya bahari ya moto huku kifo kimezuiliwa ili uteseke milele.

Mimi naamini utatengeneza ndugu baada ya kuusoma ujumbe huu.

Mimi naamini utaachana na mahawara na kuanza kuiheshimu ndoa yako.

Mimi naamini hutamsaliti tena mkeo/Mumeo.

Mimi naamini utaachana na huyo girlfriend/Boyfriend, wengine wanao zaidi ya mmoja, nakuomba ndugu achana nao.

Kijana au binti kaa tulia hadi wakati wako wa ndoa.

Uliyenisikia na utatubu na kuacha dhambi hiyo, MUNGU akubariki sana.```

ALIYE NA AKILI AWEKE MOYONI MANENO HAYA. AMINA


Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

a.gif Kila kitu ni mali ya Mungu isipokua hiki

Kila kitu ni mali ya Mungu. Kuwa na Mungu ni kuwa na kila kitu. Hata mimi mwenyewe ni mali ya Mungu. Kitu kimoja tu nina hakika nacho kwamba ni mali yangu binafsi nacho ni dhambi zanguπŸ˜›. Ee Mungu naomba niziungame niweze kubaki mali yako bila kuwa na kitu binafsi... soma zaidi

a.gif Nyimbo za Kwaresma za Katoliki

Hizi hapa nyimbo nzuri za Kwaresima zitakazokusaidia uwe na Kwaresima nzuri ya Tafakari.. soma zaidi

a.gif Nyimbo za Mama Bikira Maria

Zifuatazo ni nyimbo nzuri za Bikira Maria.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] πŸ‘‰SALA ZA KATOLIKI

[Tafakari ya Sasa] πŸ‘‰Upendo mkuu wa Yesu

[Mtakatifu wa Sasa] πŸ‘‰Mtakatifu Aloisi Gonzaga

[Jarida La Bure] πŸ‘‰Biblia Takatifu: Agano la Kale

mtu-akifa-nini-hutokea.JPG

a.gif Amri ya Kumi ya Mungu inakataza nini?

Inakataza;.. soma zaidi

a.gif Kama padri hatapatika na mgonjwa afanye nini?

Kama padri hatapatikana mgonjwa aweke nia ya kuungama na afanye majuto kamili.. soma zaidi

a.gif Liturujia inaadhimishwa wapi?

Liturujia inaadhimishwa pale waamini walipokusanyika kwa lengo hilo; kwa sababu Ibada katika Roho na Kweli ya Agano Jipya haifungwi na mahali fulani tuu, kwani dunia yote ni Takatifu.. soma zaidi

a.gif Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu… soma zaidi

a.gif Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?

Hapana, Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake… soma zaidi

a.gif X-mass inavyohusishwa na mpinga Kristo

X-MASS INAYOHUSISHWA NA MPINGA KRISTO NI TAFSIRI YA MTU BINAFSI, MWENYE MALENGO YAKE.. soma zaidi

a.gif Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?

Ndiyo, ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu wetu… soma zaidi

a.gif Je, Maria ni mama yetu pia?

Ndiyo, Maria ni mama yetu pia: kwa kushiriki kazi yote ya Mwanae, Adamu mpya, amekuwa Eva mpya, mama wa wale wote aliowakomboa msalabani… soma zaidi

a.gif Kabla ya kuungama ni lazima kufanya nini?

Kabla ya kuungama ni lazima kukusudia kuacha dhambi na kuepuka nafasi kubwa ya dhambi bila kusahau kufuata hatua sita za kabla na baada ya kupokea kupokea Sakramenti ya Kutubio ambazo ni,.. soma zaidi

a.gif Historia Fupi ya Ibada ya Rozari

Katika Kalenda ya Kanisa Katoliki,
huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi
ni miezi ambayo imewekwa kwa ajili ya
Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo
hiyo miezi huwa inasaliwa rozari.
Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa
nini ifanyike miezi hiyo? Yafuatayo nimajibu, mwezi wa tano umewekwa kwa
heshima ya Bikira Maria kutokana na
nini kilitokea katika historia hapo
nyuma… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.