Ujumbe kwa wakina dada

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

Ujumbe kwa wakina dada

Dada, Mwanaume mwenye busara hashawishiki na Uzuri ulionao, umbile lako, mawigi na mitindo ya nywele unayobadilisha kila siku, wala kwa rangi yako hiyo ya kizungu uliyoinunua dukani kwa sh 3500.

Mwanaume mwenye busara huvutiwa na Hekima, busara na maarifa uliyonayo. Uzuri wako bila Vitu hivi ni sawa na BURE, hamna kitu.

Muonekano wako wa nje utavutia wababaishaji (mashalobalo) na si Waoaji. Uzuri wako unafaa kwa matumizi ya mara moja kitandani na si kwa kuwekwa ndani.

Kweli dada ni mzuri, shape ya kuvalia Nguo unayo, hata ukivaa dela bado unaonekana, Lakini sasa unaifukuzia miaka 30 hata dalili za Ndoa hamna, unabaki kushuhudia harusi za wadogo zako miaka 20 - 22 wakiolewa.

Dada ni kweli kwa nje unaonekana mtu lakini ndani hauna kitu, upo mtupu sana, umepwaya. Haubebeki, haununuliki, wala hauuziki.

Kuna msemo usemao "Uzuri wa Mkakasi ndani kipande cha mti". Biblia pia inasema

"Mwanamke mzur asiyekuwa na HEKIMA ni sawa na Pete ya dhahabu Katika Pua ya Nguruwe" (Mithali 11 :22).

Hekima ndio kitu pekee kisichoharibika unachopaswa kujivunia nacho, hata kama bila ya Make Up, Hekima itakufanya ung'are.

"Hekima ya mtu HUMNG'ARIZA USO wake, na Ugumu wa USO wake HUBADILIKA" (Mhubiri 8 :1).

Tabia yako ndio Kikwazo chako. Mwanamke hauna nyama ya ulimi, haujui kushuka, mkali kama pilipili mbuzi kila siku hauishi Maudhi. Nani anahitaji mwanamke wa namna hii? Ni HERI ukae peke yako kwa amani kuliko kukaa na mwanamke mgomvi asiyeisha vurugu (Mithali 27 :15).

Unapenda maisha ya mtelemko, vyakula vya Supermarket kupika hautaki. Dada hivi unafikiri maisha ni movie za Kifilipino au Isidingo? Mbona una mawazo Mgando.!

Unataka mwanaume sijui mrefu, sex body, mwenye gari. Aisee, kweli..! Hekima ni ulinzi na ni zaidi ya vazi la heshima. Hilo gari Umechangia hata gharama ya kununua taili au 'site mirror'? Mbona una Vituko?

Kwa kuendekeza tamaa zisizo za msingi utatumiwa na kuachwa kama tambala la deki au Nguo ya mtumba. Nani aliyekuambia SIFA ya Mume BORA ipo kwenye kumiliki gari? Mbona unazidiwa AKILI hata Sisimizi ambaye anajua Kujitafutia?

Mwanamke mwenye busara hukubali kuanzia chini na hutafuta pamoja na Mumewe. Kuna msemo usemao UKIONA VYA ELEA, UJUE VIMEUNDWA. Na mtaka cha Uvunguni sharti Ainame.

Ngoja nikupe mfano HALISI labda utanielewa kama una kichwa cha KUELEWA. Hivi karibuni tulisikia ndoa ya Mkurugenzi wa IPP MEDIA na Keyln.

Unafikiria kwanin Mengi alimuoa Keyln? Ni kwa sababu ya Uzuri alionao Keyln? La hasha! Kama ni Uzuri, Mr Mengi hakushindwa kuwa na mwanamke yoyote mzuri anayemtaka.

Niliwahi kusoma kwenye mtandao fulani wa kijamii kuhusu habar hii, Mr Mengi alisema sababu ya kumuoa Keyln ni Hekima aliyonayo na namna anavyojua kukaa Katika nafasi yake kama Mwanamke.

Keyln alikuwa anampikia chakula yeye mwenyewe na si kutaka chakula cha supermarket, alikuwa anamfulia Nguo kwa mikono yake mwenyewe na si kwa washing machine kwa kisingizio kuwa kucha zitakatika au mikono itachubuka.

Sasa kwa huduma hizi ZOTE, ukiongezea na Uzuri alionao, kwanini Mzee asiweke chombo ndani? Hapa hakuwa na ujanja.

Sasa kama ungekuwa wewe na akili yako hiyo ya bandia, si ungeona mgodi umekudondokea. Chakula ungekuwa umeweka order ya mwaka mzima NAKUMAT supermarket.

Nguo zingekuwa zinafuliwa Marekani, zinaanikwa na kunyoshwa Paris Ufaransa, na zinarudishwa kwa ndege Tanzania. Aisee..! Hapa upele ungempata Mkunaji.

Shika point hii ya mwisho, HAIJALISHI mwanaume awe na PESA kiasi gani, atahitaji kula chakula chako na si cha housegirl au supermarket, atahitaji kuona unamfulia Nguo zake na si kufuliwa na dobi, housegirl au washing machine.

Kuingia kwenye Ndoa TU mtihani, JE UTAWEZA kulea Mume wewe..?

Hahaha, fundo limempata mfundaji.. Kazi kwako hapo, kusuka au Kunyoa. Mimi NIMEMALIZA…!Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Ujumbe kwa wakina dada

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Ujumbe kwa wakina dada

a.gif Mambo makubwa yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika

Zifuatazo ni sababu kubwa za msingi zinzozifanya ndoa nyingi za kizazi cha Leo kuvunjika haraka na kukosa kudumu.. soma zaidi

a.gif Jifunze kupitia mfano wa huyu mwalimu na wanafunzi wake

Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili hivyo hivyo… soma zaidi

a.gif Mambo ya Msingi Unayopaswa kufahamu kuhusu Ekaristi Takatifu: Mwili na Damu Ya Bwana Wetu Yesu Kristu

Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, katika
maumbo ya mkate na divai. Sakramenti hii
iliwekwa na Yesu Mwenyewe kwenye karamu ya mwisho, siku ya Alhamisi jioni kabla ya mateso
yake. (Yoh 6:1-71; Mt 26:26-28)... soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Karoli - Nipe Biblia

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala ni Upendo

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Margareta Maria Alacoque

SASA.gif

a.gif Je, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi?

Ndiyo, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi tulizotenda baada ya ubatizo, kwa kuwa hatuwezi kupokea msamaha tukikataa masharti yake, na Mungu ametupangia watu ambao watuondolee kwa niaba yake… soma zaidi

a.gif Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu… soma zaidi

a.gif Kilele cha Liturujia ni nini?

Kilele cha liturujia ni Sadaka Takatifu ya Misa.. soma zaidi

a.gif Je, ni muhimu tujiandae kufa?

Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Eb 9:27)… soma zaidi

a.gif Kujinyima ni nini?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k… soma zaidi

a.gif Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;.. soma zaidi

a.gif Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?

Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la… soma zaidi

a.gif Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?

Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa… soma zaidi

a.gif Muamuzi wa Mwisho ni Mungu

Mungu ndiye Muamuzi;.. soma zaidi

a.gif Haleluya Msifuni MUNGU

Haleluya. Msifuni MUNGU katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la
uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa
kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na
kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; Msifuni
kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi
yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu
BWANA. Haleluya''… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.