Tumia kile ulichonacho kwa sasa Ndio baraka aliyokupa Mungu, usingoje miujiza

By, Melkisedeck Shine.

Mungu angetaka kukufanyia kila kitu asingekupa miguu ya kutembelea, asingekupa mikono wala macho ya kuona na masikio ya kusikia. Asingekupa akili ya kufikiria na wala asingekupa nguvu za kufanyia kazi. Angekufanyia kila kitu na wewe kukaa tu, ana uwezo huo na angeweza kufanya hivyo lakini hakufanya.

Lengo kuu la Mungu kukupa hivyo vitu ulivyonavyo nikwasababu yeye huanzia pale miguu yako inapoishia kutembea, huanzia pale mikono yako inaposhindwa kushika, pale macho yako yasipoweza kuona, pale ambapo masikio yako hayawezi kusikia na kubwa zaidi pale ambapo akili yako inapoishia kufikiria ndipo nguvu zake huhitajika.

Acha kukaa tu na kusubiri Mungu atende, kuishi kwenye maombi ukiomba baraka zake huku ukiwa hufanyi chochote. Kama unamjua Mungu vizuri basi ungejua kua tayari ameshakupa baraka unazoziomba amekupa baraka ya Mikono, itumie, kashakupa baraka ya miguu, kashakupa baraka ya macho, masikio, akili na nguvu ya kufanya kazi.

Nibaraka nyingine ipi tena unaanza kuomba kama hiyo aliyokupa sasa umeshindwa kuitumia. Unadhani ni wangapi ambao wanaomba kuwa kama ulivyo sasa na Mungu bado hajaamua kuwabariki. Hembu jiulize hutumii mikono yako kufanya kazi, miguu yako kufanya kazi unaomba Mungu akuletee chakula vipi yule ambaye hana mikono au miguu.

Una afya njema umekaa tu nyumbani unalalamika vipi wale waliopo mahospitalini. Wao wanahitaji kumuomba Mungu kuwapa afya kwanza kabla ya kumuomba baraka nyingine wewe tayari unayo baraka ya afya lakini bado unalalamika. Mshukuru Mungu kwa baraka alizokupa, zitumie vizuri na muombe akuongoze katika kuzitumia.

Acha kusema kila kitu unamuachia yeye wakati tayari kashakubariki, tumia baraka alizokupa kwa kadri ya uwezo wako na elekeza sala zako katika kumuomba yeye kuanzia hapo ulipoishia, pale ambapo huna uwezo napo. Mshukuru kwa kutumia alivyokujalia kuwa mtu bora zaidi na si kwa kulalamika kila siku kuwa huna bahati wakati kuzaliwa jinsi ulivyo ni bahati kubwa.Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Tumia kile ulichonacho kwa sasa Ndio baraka aliyokupa Mungu, usingoje miujiza

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Tumia kile ulichonacho kwa sasa Ndio baraka aliyokupa Mungu, usingoje miujiza

a.gif Jifunze kitu kupitia mkasa huu wa kusisimua

Kulikua na bwana👤mmoja masikini sana😳😳Kutokana na dhiki kumwandama ilifikia wakati alitamani kufa😮kuliko kuendelea kuishi sehemu alipokuwa anaishi kulikuwa na
msitu🌵🌱🌿🌴🌲mkubwa ambao ndani yake linaishi zimwi👹👹👹lenye kula watu na katika msitu huo hajawahi kuingia binadamu👴 akarudi salama✌wote waliliwa na zimwi👹👹.. soma zaidi

a.gif Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

MKASA WA KUSISIMUA : MUNGU AKIPANGA KUKUINUA HAMNA ATAEWEZA KUZUIA, HATA SHETANI HATOWEZA… soma zaidi

a.gif Nafasi ya Bikira Maria Katika Kanisa Katoliki

Kanisa katoliki linamthamini Bikira Maria kama Mama wa Mungu, Mama wa Kristu, Mama wa Mkombozi pia Mama wa uhai kuna maneno kadhaa hutumika pia kufafanua zaidi hiyo heshima mfano HYPERDULIA zaidi ya…. Bikira Maria tunamheshimu zaidi ya watakatifu, PROTODULIA ikiwa na maana ya heshima kwa Bikira Maria zaidi ya Mt. Yoseph na pia LATRIA likiwa na maana ya heshima kwa Mungu peke yake kwani ndani yake kuna kunakuabudu pia!!!.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALAMU MARIA

[Wimbo Mzuri PA.gif] Uwinguni ulipo Mama

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa Mungu hauna mwisho

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Maria Goretti

UJUMBE-POLE-NDUGU.JPG

a.gif Katika Amri ya Tano ya Kanisa tumeamriwa nini?

Katika Amri ya Tano ya Kanisa tumeamriwa kufahamu kuwa gharama za dini na za mapadre zatupasa. Yaanai wakristo walitegemeze Kanisa na wahudumu wake na hasa katika kazi ya kueneza injili… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Daraja ndiyo nini?

Sakramenti ya Daraja ndiyo Sakramenti ambayo mwanamme mkatoliki aliyeitwa na Mungu hupata mamlaka na neema ya kuendeleza ndani ya Kanisa Utume Kristo aliowakabidhi Mitume wake.. soma zaidi

a.gif Kishawishi ni nini?

Kishawishi ni tamaa au mvuto mbaya wa kwenda kinyume na Mapenzi ya Mungu ili kuvunja Amri zake na za Kanisa lake… soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu, kwa nini Mungu hatendi mpaka umwambie au umuombe?

Mungu anapenda kutenda jambo baada ya mtu kumuomba/kusali ili mtu aelewe Ukuu wa Mungu na ili Mungu atukuzwe… soma zaidi

a.gif Lengo kuu la visakramenti ni lipi?

Lengo kuu la visakramenti ni kuwaandaa watu wapokee kwa imani sakramenti zitakazowatia uzima wa Mungu unaodumu milele. Hivyo visakramenti visitiwe maanani kuliko sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe ziwe kiini cha maisha yetu… soma zaidi

a.gif Wakati wa Sakramenti ya Kitubio Utamwomba Roho Mtakatifu kwa sala gani?

Utamuomba Roho Mtakatifu kwa sala hii:.. soma zaidi

a.gif Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?

Ndiyo, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele… soma zaidi

a.gif MAANA YA SALA KWA MKRISTO

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Inatupasa kusali kila siku bila kukata tama kwa ibada, kwa matumaini na kwa saburi. Kama mfano Yesu Alitufundisha sala ya Baba yetu.
Yatupasa kuwaombea wengine, watu wote wenye shida wakosefu na hata maadui zetu, vilevile tumtolee Mungu shukrani kila wakati na hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu… soma zaidi

a.gif Ina maana gani kupaka mafuta ya Krisma katika panda la uso wakati wa Kipaimara?

Inamaana kuwekwa wakfu (Yh 17:16-17)… soma zaidi

a.gif Baba Mtakatifu ni nani?

1. Ndiye Askofu Mkuu wa Maaskofu wote.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.