Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

MKASA WA KUSISIMUA : MUNGU AKIPANGA KUKUINUA HAMNA ATAEWEZA KUZUIA, HATA SHETANI HATOWEZA.

#inasikitisha

Mama Haulat baada ya mme wake kufariki ndugu wa mme walimnyang'anya mali zote na kumfukuza katika nyumba yake. Hakuwa na pa kukimbilia hasa ukizingatia kuwa kwa bahati mbaya zaman alikuaga mtoto wa mitaani kabla ya kuolewa na baba yake HAULAT hivyo hakuwa na ndugu wa kumtetea . Mama Haulat alilia sana ila haikusaidia, ndugu wa mme wote walimgeuka hivyo akaondoka na mwanae Haulat na kurudi maisha yake ya awali ya kuishi kwenye makalafati na chini ya madaraja ambapo ndio makazi ya watu masikini wasio na makazi. Alimlea mwanae kwa shida ivyo ivyo chini ya kalafati mmbu waliwauma mno, magari ya takataka yalikua yakimwaga takataka ikiwemo vinyesi na shombo jirani na kalafati lao harufu ilikua kali mno ila iliwalazimu kuizoea.

Mama Haulat alikua akimwambia mwanae kwa uchungu kuwa MUNGU ALIYENITOAGA HUKU NIKIWA MTOTO WA MTAANI NA KUNIKUTANISHA NA BABA YAKO NIKAOLEWA NIKAKUZAA TUKAISHI KWA FURAHA ILE, ATATUKUMBUKA NA KUJA KUTUTOA WOTE TENA. Haulat alifarijika sana kwa maneno yale ya faraja ya mama yake yaliyompa tabasamu siku zote na kujiona wa thamani japo jamii ilikua ikiwadharau mno.

Alimpeleka shule moja ya msingi ilioko jirani nao katika mji ule wa Mumbai nchini India. Shuleni Haulat alikuwa akichukiwa sana na walimu wake wa darasa. Haulat alikuwa akijitahidi kufanya kila jambo kuwafurahisha walimu wake lakini walimu walizidi kumchukia kuliko wanafunzi wao wote. Haulat alipofika darasa la 4,
Siku moja wamisionari tokea Marekani walitembelea shule ya kina Haulat na wakataka mtoto mmoja aliopo darasa la 4 ili waende nae Marekani akasome huko na kumfadhili masomo yake mpaka chuo kikuu. Kwa kujua hili mwalimu wa darasa la kina Haulat alimweka HAULAT mwishoni kabisa mwa darasa akae huko ili watakapoingia wale wafadhili wasipate kumchagua. Aliambiwa KAA HUKU NYUMA USIJETUTIA AIBU SHULE YETU KWA WAGENI NA MIHARUFU YAKO YA JALALANI, MCHAFU SANA WEWE akamtia na kwenzi moja la msisitizo.
Wamisionari walipoingia darasani, waliongea na wanafunzi wote na mmoja wao akaenda nyuma ya darasa, alimuona binti mmoja dhaifu mwenye sura ya huzuni kuu, kumbe alikua Haulat,
Sura ya Haulat ilionyesha unyonge na huzuni sio kwa ajili ya wageni wale bali manyanyaso aliyopewa na mwalimu wa darasa na lile kwenzi la msisitizo hivyo alikua akisikitika na kuhisi Mungu amemsahau dunia inamdhalilisha. Ghafla pasipo yeyote kutarajia,
Kutoka kule alimteua HAULAT kuwa mwanafunzi atakaenufaika na ofa ile ya kwenda Marekani kusoma. Hivyo basi ingawa HAULAT aliwekwa mwisho kabisa mwa darasa lakini akawa wa pekee na kupata ofa ile ya kwenda kusoma. Aliwaeleza hali yake na mama yake wafadhili wale wakakubali kumchukua Haulat na mama yake akaishi Marekani.
Alisoma na kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, na mpaka hivi sasa ni mwanasheria katika kampuni moja ya uwakili huko New Jersey Marekani.

FUNDISHO :
Hakuna binadamu atakaetibua Mipango ambayo Mwenyezi Mungu amekupangia. Mipango ya adui zako kuzuia baraka zako haitafanikiwa kamwe. Siku zote utakuwa wa kwanza na sio wa mwisho.
Nakutakieni heri ya mafanikio na fanaka katika shughuli zenu halali zinazowaingizieni kipato.
Kwanini usiseme AMEN! kupokea sala hii.
.Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

a.gif Nafasi ya Bikira Maria Katika Kanisa Katoliki

Kanisa katoliki linamthamini Bikira Maria kama Mama wa Mungu, Mama wa Kristu, Mama wa Mkombozi pia Mama wa uhai kuna maneno kadhaa hutumika pia kufafanua zaidi hiyo heshima mfano HYPERDULIA zaidi ya…. Bikira Maria tunamheshimu zaidi ya watakatifu, PROTODULIA ikiwa na maana ya heshima kwa Bikira Maria zaidi ya Mt. Yoseph na pia LATRIA likiwa na maana ya heshima kwa Mungu peke yake kwani ndani yake kuna kunakuabudu pia!!!.. soma zaidi

a.gif Mungu ni Mkubwa kiasi gani

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake. "Baba, hivi Mungu ni mkubwa kiasi gani?" Baba yake akatazama juu angani akaona ndege ya abiria akamuuliza mwanae "mwanangu, ile ndege ina ukubwa Gani?" Mtoto akajibu ni ndogo sana.
Basi Baba yake akamchukua hadi uwanja wa ndege walipofika karibu na ndege akamuonesha ndege akamuuliza " ile ndege ina ukubwa gani?? Mtoto akajibu "Hiyo Ndege ni Kuuuubwa sana" basi Baba yake akamwambia.. soma zaidi

a.gif Vitabu vya Historia katika Biblia ni vipi?

Vitabu vya Historia katika Biblia ni
1. Yoshua
2. Waamuzi
3. Ruthu
4. 1 Samweli
5. 2 Samweli
6. 1 Wafalme.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Bwana alivyo mkarimu

[Tafakari ya Sasa] 👉Neno "Nimekusamehe"

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Margareta Maria Alacoque

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

baada-ya-kufa.JPG

a.gif Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?

Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15).. soma zaidi

a.gif Matokeo ya hukumu hiyo ni nini?

Matokeo ya Hukumu hiyo ni roho kwenda Mbinguni, Toharani au Motoni. (Mt 25:34-46).. soma zaidi

a.gif Nini maana ya neno "Fumbo"?

Fumbo ni ukweli ambao hatuwezi kuelewa kikamilifu, lakini tunasadiki kwa kuwa Mungu hutufumbulia. (Math 11:27).. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Kipaimara ni nini?

Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu upendo

Katika fadhila zote, upendo ndio unaonyesha uwepo wa fadhila nyingine.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Utatu Mtakatifu

Haya hapa Maswali na majibu kuhusu Utatu Mtakatifu;.. soma zaidi

a.gif Kanuni za kuishi maisha ya ushindi na baraka

MWL Gasto Joachimu.
Wakat wa kung'ang'ana na Baraka ambazo Mung ameamuru Maishan mwako ni sasa mpendwa
Yakobo alingangana na malaika had akambariki.Uko wap ewe yakobo wa sasa?
Wakati wa kulisimamisha jua ni sasa maana ushind wetu nileo🌺🌺🌺Yoshua alijua ushind wake uko wakati ule… soma zaidi

a.gif Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;.. soma zaidi

a.gif Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

Angalizo; Tunapoongelea kuhusu pombe sio kwamba tunahamasisha kutumia pombe bali tuelewe kile tunachofanya kwa mapenzi ya Mungu!
pombe haikukataliwa ila itumike kwa kiasi… soma zaidi

a.gif Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu ngapi?

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanywa katika sehemu 4 nazo ni
1. Vitabu vya Musa (5)
2. Vitabu vya Historia (16).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.