Usifanye maamuzi kwa kutumia vigezo vyepesi.
"Nampenda sana"
"Tunapendana mno"
Unaweza kumpenda mtu yeyote. Upendo huzaliwa na huuawa na mazingira fulani. Kwamba unampenda (sana) sio jambo la msingi.

Usifanye maamuzi kwa sababu umechanganywa na umbile lake. Umbile linazoeleka. Umbile linapita. Baada ya muda fulani hutaona thamani ya hilo umbo linalokunyima usingizi leo.

Usiifanye kazi kuwa kigezo. Heshima ya kifedha aliyonayo leo inaweza kupotea wakati wowote. Unayemwona 'amechoka' leo, kesho anaweza kukushangaza.

Hapa sikushauri. Nakupa taarifa. Uamuzi ni wako.
Uhusiano imara kati ya watu wawili unajengwa kwenye msingi imara:

1. Kukubaliana kwenye MAMBO YA MSINGI. Imani. Dini. Misimamo. Mambo gani unayachukulia kuwa ya muhimu zaidi kwako? Mambo gani hayana mjadala kwako? Kitu gani huwezi kukivumilia? Usipuuze tofauti kati yetu kwenye mambo ya msingi. Huwezi kufika mbali na mtu mnayependana lakini mkitofautiana kwenye masuala muhimu.

2. Uwezo wa kuelewa na KUTHAMINI MAHITAJI ya wengine. Wakati mwingine utalazimika kufurahia kufanya kitu usichokitaka au hata kuacha unachokitaka kwa sababu tu unajua kufanya hivyo kutamgusa mwenzako. Huu unaitwa UKOMAVU, kinyume kabisa cha ubinafsi. Kama mmoja wenu bado anajifikiria mwenyewe, hamjawa tayari bado.

3. Kufahamiana. Ukimfahamu mtu itakusaidia kufanya maamuzi yanayoongozwa na uelewa. Upendo unapofusha macho. Unahitaji muda kuhamishia upendo kutoka machoni kwenda akilini.

Kwamba anakuheshimu sana haimaanishi ana heshima. Namna gani anaheshimu wahudumu wa mgahawa wa chakula, walinzi wa geti, makondakta na hata watu wasio msaidia? Huwezi kuyasaili hayo kwa kukurupuka. Jipeni muda wa kufahamiana.

4. Hutafuti malaika. Wewe mwenyewe wengi wanakuvumilia. Una mapungufu mengi hata kama hawakwambii. Kiburi kisikufanye ujione una haki ya KUMPATA mwenye sifa usizonazo. Kama wewe umewahi kukosea, kwa nini unatafuta asiyekosea? Hiyo, hata hivyo, haimaanishi upuuze mambo ya msingi.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare posti hii.πŸ‘ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!πŸ’―βœ”

ml.gif

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..
Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>
MELKISEDECK-SHINE-LEON.jpg

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine,

Tafakari leo kwa kusoma Biblia kitabu cha Luka 6:20-49. Huu ndio msingi wa Mkristo, maana ya kuwa Mkristo na tofauti ya Mkristo na asiyemkristo.

Mungu Akubariki sana…. Tuzidi Kuombeana na kujitahidi kuishi kama alivyotufundisha Yesu Kristo Ili tuweze kumfikia yeye.