Zifuatazo ni sababu kubwa za msingi zinzozifanya ndoa nyingi za kizazi cha Leo kuvunjika haraka na kukosa kudumu

(1) KUKOSEA KUOA/KUOLEWA NA YULE MWENZA SAHIHI WA MAISHA YAKO

Biblia inatuambia katika MWANZO 2:18:-" BWANA Mungu akasema, si vema mtu huyu awe pekee yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye"

Unajua ukioa/kuolewa na mtu yule ambaye hamfanani naye. Kitakachokuja kutokea hapo mbeleni, lazima kila hiitwapo leo mtapishana sana, mtagombana , mtasuguana sana na mwisho wa siku mtaachana soremba.

Hii ni mojawapo ya sababu kubwa zaidi ya ndoa nyingi kuvunjika.

Kutokumuoa mke/mume ambaye hamfanani naye. Mwisho wa ndoa hiyo lazima itavunjika tu.

Ndiomaana ni muhimu sana kumwomba Mungu akupe na akuoneshe mwenza sahihi wa kufanana nawe. Na ukifanikiwa kumpata ndoa yako itadumu kwa maisha ya furaha.

(2) KUKOSEKANA KWA HOFU YA MUNGU

[ MITHALI 8:13 ]

Hili mojawapo ya tatizo jingine kubwa sana ambalo limesababisha ndoa nyingi kuvunjika nyakati hizi za Leo.

Unajua ukiwa na hofu ya Mungu. Huwezi kumsaliti mkeo au kumtendea vibaya kwa namna yoyote ile.

Bali utakuwa mkweli na mwaminifu kwake, utampenda na kumthamini .

Kama wanandoa wote mkiwaa mmejaa *hofu ya Mungu* mioyoni mwenu kweli kweli. Ndoa yenu itadumu katika hali ya amani na utulivu siku zote za maisha yenu.

(3) KUKOSA HEKIMA

Hekima ni kitu muhimu sana katika ndoa.

Hekima itakufundisha vizuri jinsi ya kumjibu mmeo na ujibu vipi na kwa wakati upi.

Hekima itakusaidia jinsi ya kuishi na mmeo/mkeo hata kama yeye ana udhaifu na mapungufu mengi kiasi gani.
Hekima itakusaidia jinsi ya kuishi naye

MITHALI 14:1:-" Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliyempumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe".

1 PETRO 3:7:-" Kadhalika ninyi waume, *kaeni na wake zenu kwa akili*; na kumpa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe".

Hekima itakufundisha uishi vipi na mkeo au mmeo na wote wanaokuzunguka.

Kukosekana kwa hekima. Hii ni mojawapo ya sababu kubwa sana zilizopelekea ndoa nyingi kuendelea kuvunjika na kuzidi kuvunjika.

(4) KUKOSEKANA KWA ROHO YA UNYENYEKEVU NA UVUMILIVU

[ 1 PETRO 3:8-9; WAKOLOSAI 3:12-14 ].

Kinachotofautisha ndoa za zamani zilizodumu na ndoa za kizazi sasa . Ni hii point.

Taasisi ya ndoa ndani yake huwa kuna changamoto nyingi za hapa na pale.

Ndoa za wazee wetu zilidumu sana muda mrefu mpaka kifo . Kwa sababu walijua sana kuvumiliana.

Na pia wanawake wa zamani walijua sana na kufundwa vizuri jinsi ya kushuka chini ya waume zao (unyenyekevu).

Lakini mabinti wa ki-leo kizazi cha dotcom sometime kwa sababu ya kiburi chao cha usomi au pesa. Yaani Wakiolewa, *wanajiona sana wao ndio wao* na ile ya kumnyenyekea mume inaondoka. Watapenda sana kuwapanda vichwa waume zao.

Na tena hiii Sera ya 50 KWA 50 Ndiyo imewavimbisha kichwa kabisaa wanawake na kuwaharibu . Yaani mwanaume hana tena sauti ndani. Mume akisema na mke anasema. Hakuna wa kujishusha na kutii Sasa hapo Unashindwa kuelewa kati ya mwanaume na huyu mwanamke, nani ndio kichwa ndani ya nyumba !!

Ndoa yoyote ile ikikosa ile roho ya unyenyekevu na uvumilivu miongoni mwa wanandoa. Ndoa kama hiyo lazima itavunjika.

(5) KUTOKUWA NA MAISHA YA MAOMBI MIONGONI MWA WANANDOA

[ ZABURI 32:6; MATHAYO 26:40-44]

Maombi ni kitu muhimu sana kwa wanandoa. Na kama wanandoa hawana maisha ya maombi mbele za Mungu. Ni rahisi sana ndoa hiyo shetani kupata nafasi ya kuivuruga na kusambaratisha haraka.

[ LUKA 22:31-32 ]

Maombi ndio njia pekee inayomfanya Mungu aihatamie, aitawale na kuiongoza ndoa yako.

[ ZABURI 32:8 ]

(6) ROHO YA KUTOKURIDHIKA

[ 1 TIMOTHEO 6:6-8 ]

Mwenzako anajitahidi kukufanyia kila unachokihitaji mwanamke/mwanaume, lakini bado huridhiki hata hapo .

Sasa wewe unataka afanyeje ? Enhee!!

Unamlazimisha kufanya vitu ambavyo hata hana uwezo navyo.

Hii ni moja ya sababu kubwa pia inayochangia ndoa nyingi kuvunjika.

(7) ROHO YA TAMAA

[ WAEFESO 5:3-5; 1TIMOTHEO 6:9-10 ]

Nayo ni chanzo kikubwa cha ndoa nyingi kuendelea kuvunjika kila hiitwapo Leo.

(8) KILA MMOJA KUTOKUJUA KUSIMAMA KWENYE NAFASI YAKE

Katika maisha ya ndoa mke na mume kila mmoja ana majukumu yake ambayo amepewa na Mungu ahakikishe anayatekeleza kikamilifu wajibu wake.

Kwa mfano

Baadhi ya mojawapo ya majukumu

Mwanaume amepewa jukumu la kumpenda sana na kumtunza mkewen.k.

Mwanamke amepewa jukumu la kumtii na kumpendeza mume wake katika mambo yote n.k.

[ WAEFESO 5:22-33 ]

Sasa pakiwa na Muingiliano wa majukumu. Mke anataka kusimama kwenye nafasi ya mume na mume anataka kusimama kwenye nafasi ya mke ndani ya nyumba. Sasa hapo lazima ndoa itayumba na kuelekea kupooromoka.

πŸ™‰πŸ™‰πŸ™‰Usisahau kushare makala hii kuhusu Mambo makubwa yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika.πŸ‘ Share facebook, twitter n.k bila kusahau WhatsApp!πŸ’―βœ”


IMG_20170703_130936.jpg
Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Uwe na subira Baada ya kuomba kwa Mungu. Sio kila unachoomba kwa Mungu utakipata kwa wakati huo huo au kwa wakati unaofikiri. Mungu ni Mwaminifu Sana Kwenye kujibu maombi lakini vile vile ni mwenye Hekima Kwenye kukujibu, anajua wakati gani ni sahihi kukujibu maombi yako. Anaweza kukujibu saa hiyo hiyo, kesho, keshokutwa au hata mwakani kwa kuangalia wakati ufaao na kwa manufaa yako. Kwa hiyo unapoona hujajibiwa usife moyo, bali uwe na matumaini. Mungu anajua akujibu lini kwa kuwa anajua ni lini wakati ufaao na ni lini kitu kipi kina kufaa.

Mungu Akubariki sana… Tuombeane!

ml.gif

πŸ“š Endelea kusoma kuhusu;-πŸ‘‡

Ndugu.gif