Madhara 6 ya kutoa Mimba

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

Madhara 6 ya kutoa Mimba

Kutoa mimba ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.

Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

1. Uwezekano mkubwa wa kufa:

Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

2. Ugumba kwa wanawake wengi:

Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

3. Mimba kutunga nje ya kizazi:

Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

4. Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:

Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

5. Kansa ya mlango wa uzazi:

Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

6. Kuathirika kisaikolojia;

Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho

kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba…maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..kwa maelezo zaidi.
Frt. Lujwangana AntidiusFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Madhara 6 ya kutoa Mimba

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Madhara 6 ya kutoa Mimba

a.gif Faida ya kuabudu Ekaristi Takatifu

1.Kila saa moja tunayotumia kuabudu, inafurahisha moyo wa Yesu na hivyo majina yetu huandikwa mbinguni kwa ajili ya uzima wa milele (Mama Thereza wa Calcuta).. soma zaidi

a.gif Hii ndiyo maana ya msemo Wema hauozi

Kuna mwanamke tajiri alikuwa akiendesha gari lake, katikati ya njia gari likaharibika, akateremka na kuomba lifti, lakini magari yalikuwa yanampita bila kusimama… soma zaidi

a.gif Matumizi ya Neno 'Ameen'

Napenda kuchukua fursa hii kutoa mchango wangu juu ya matumizi mabaya ya neno "Ameen. " Hili neno linatokana na neno la Kiebrania "Amina" likiwa na maana ya "Na iwe hivyo." Neno hilo lilitumika mwishoni mwa maombi kila wakati Wayahudi walipomwomba Mungu wao… soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa Mungu hauna mwisho

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

UJUMBE-WA-ZA-JIONI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Faida ya kupanga taratibu za ibada ni ipi?

Faida ya kupanga taratibu za ibada ni hasa kuhakikisha yote yafuate usahihi wa imani na maadili, yakidumisha umoja na upendo, badala ya kumuachia kiongozi au mwingine yeyote aseme na kufanya anavyotaka. Mitume wenyewe walianza kazi hiyo, wakidhibiti hata karama… soma zaidi

a.gif Nyimbo za Mama Bikira Maria

Zifuatazo ni nyimbo nzuri za Bikira Maria.. soma zaidi

a.gif Kujikweza Mbele ya Mungu

Rejea Luka 14:7-24 na Luka 18 :9-18.. soma zaidi

a.gif Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani… soma zaidi

a.gif Tumia kile ulichonacho kwa sasa Ndio baraka aliyokupa Mungu, usingoje miujiza

Mungu angetaka kukufanyia kila kitu asingekupa miguu ya kutembelea, asingekupa mikono wala macho ya kuona na masikio ya kusikia. Asingekupa akili ya kufikiria na wala asingekupa nguvu za kufanyia kazi. Angekufanyia kila kitu na wewe kukaa tu, ana uwezo huo na angeweza kufanya hivyo lakini hakufanya… soma zaidi

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Je, Baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima kuendelea kujifunza Dini?

Ndiyo, Baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima kuendelea kujifunza Dini ili tuweze kuelewa na kulinda Imani yetu na kutumia vema neema ya Kipaimara… soma zaidi

a.gif Kanisa ni la Kimisionari maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kimisionari maana yake limetumwa kupeleka habari njema kwa mataifa yote. (Mt 28:19-20).. soma zaidi

a.gif Mitego ya Shetani katika maungamo

Katika maungamo ni lazima kuwa wanyenyekevu na wanyofu. Shetani daima anatuwekea mtego wa aibu, ni lazima tuutegue. Baadhi ya aibu anazotuwekea shetani ni pamoja na:.. soma zaidi

a.gif Kanisa ni la Kitume maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kitume maana yake wakubwa wake yaani Baba Mtakatifu na Maaskofu nimahalifa wa Mitume.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.