YESU%20MFALME%20WA%20HURUMA.gif

Blog kwa Wakatoliki

Mpangilio wa kurasa Kwa Wakatoliki ndani ya AckySHINE

|| HOME || MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

.

👉 Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke✅

Melkisedeck

Msomaji wangu mpendwa, asante kwa kuendelea kupenda kutembelea blog hii. Baada ya kukuandalia makala kuhusu;

Leo nimekutayarishia makala kuhusu Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke.

Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke

NDOA sio kichaka cha kujificha kukimbia matatizo. NDOA sio mahali pa kutolea mkosi. Wala sio mahali pa kupunguzia shida. Ndoa sio mbadala wa elimu na michakato ya kimaisha. Huolewi ili kupunguza adha za maisha. NDOA ni jukumu zito kuliko hata kusoma masters degree ya Neuro-surgeon. Wengi hamjaweza kumudu maisha yenu binafsi na bado mnalilia Mungu kuwaongezea jukumu la kumeneji maisha ya mtu mwingine.

Kama huwezi hata kujitafutia hela ya kusuka nywele zako utawezaje kuendesha maisha ya familia. Maana unaweza kuolewa na mwanaume mwenye pesa lakini akapitia mithihani pesa zikatoweka utafanyaje kama huna akili ya kujiongeza? Ndio maana wengi mnawakataa watu wenye Ndoto lakini hawanapesa kwa sasa kwa sababu ya akili ya utegemezi. Unataka mwanaume mwenye kila kitu, sababu kubwa ni uvivu na uzembe. Hutaki kujitafutia vya kwako.
Ukisoma MITHALI 31 inaeleza habari za MKE MWEMA.

Hapo ndio pa kujipima je unakidhi hivyo viwango? Mke mwema sio tegemezi ila ni mwanamke mwenye uhuru wa kifedha (Financial Freedom). JIULIZE TU KAMA IKITOKEA HUJAOLEWA MIAKA MITANO IJAYO UTAKUWAJE? MAISHA YAKO YATAKUWAJE? UTAKUWA NA HALI GANI? Maswali kama haya yatakusaidia kujiongeza. Tafuta kitu cha kufanya hata kama Ndoa isipotokea leo isiwe mwisho wa maisha, Ndoto na maono yako. Siku hizi wanaume hawaulizi ukoo wanauliza UNAFANYA NINI?

Mtu anapiga hesabu akikuoa mkaunganisha nguvu mtafanya nini kwenye maisha. Sasa wewe kalia kubandika kope na kuchora kucha kutwa nzima huna shughuli ya kufanya huku ukingoja kuombewa upate Mume. Watu hawaoi mapambo wanataka Wake watakao tengeneza nao hatma zao. Pambo ni kwaajili ya Starehe lakini MKE ni kwaajili ya maisha. Sikupondi wala sio nia yangu kukuvunja moyo, nataka utoke hapo ulipo ujiongeze ili hata ukiingia kwenye Ndoa isijae visa na kuonewa. Pesa itakupa heshima, pesa inakupa sauti, hata Wakwe zako hawawezi kukunyanyasa ukiwa na pesa kwani wanajua watakosa vitenge.

Nataka nikwambie kweli, ukiwa na hela utachagua mwanaume wa kukuoa kwani wapo wengi ila kama umefulia, tegemezi kweli utaona wanaume ni wachache. Pata kitu cha kufanya, tengeneza milango ya kipato. Badala ya kukesha unaomba Mungu akupe Mume anza kuomba Mungu akupe uhuru wa kifedha, kama itakubidi kurudi shule rudi tu. Jiongeze usibaki hapo ulipo. Ni Yesu peke yake asiyebadilika (Hebrania 13) Lakini wanadamu wote lazima tubadilike kila kukicha tukihama hatua moja kwenda nyingine.

Mungu akufungue macho kuona kiini cha ujumbe huu na lengoF lake na wala usichukuliwe na upepo wa adui upindishao maana katika jumbe zenye kubadilisha maisha kama hii.

Kuolewa sio mwisho wa maisha, Mungu kwanza achukue nafasi kwenye maisha yako na akupe utoshelevu katika moyo wako kiasi kwamba uone hata bila Mume unaweza kuishi.

[NZURI HII👉] Kuumbwa kwa Dunia

Melkisedeck

Nitumie Maoni yako Kuhusu Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke hapa

Jina
Dini/dhehebu
Mfano Mwislamu, Katoliki, Lutherani, Mlokole n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako


🙉Usisahau kushare posti hii Kuhusu 👉Maana halisi ya kuolewa au ya kuwa mke, Share✔ Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp n.k..💯✅

📚 Endelea kusoma kuhusu;-👇

Huruma ya Mungu ni ya Milele na Upendo wake ni Wa DAIMA!

Mungu ni mwenye Huruma, Rehema na Neema. Anataka watu wote waokolewe na Wala sio Hakimu na Mtoa Adhabu. Soma zaidi...

Mimi naitumainia Huruma ya Mungu
Wewe je?

Ifahamu Huruma ya Mungu hapa>>>

Karibu uonje Huruma ya Mungu Baba yetu iliyo tunda la Upendo wake Mkuu Kwetu. Utasitasita mpaka lini? Wakati wa Kubadili Maisha ni sasa

Soma zaidi kuhusu Huruma ya Mungu Hapa na jinsi ya kuipokea na kuitumainia>>>

.

.

.

Melkisedeck

Tumsifu Yesu Kristu…

Jina langu ni Melkisedeck L. Shine. Mimi ni Mkristu Mkatoliki
Karibu Katika Blog yangu ya Kikatoliki mahali pa kusoma makala mbalimbali za Kikatoliki, sala, Tafakari, Picha za Katoliki pamoja na nyimbo za Kikatoliki

Blog ya AckySHINE Kwa Wakatoliki ni Blog pekee ya Kiswahili ya Kikatoliki kwa posti nyingi, isiyochosha kusoma, yenye posti nyingi nzuri mpya kila saa unapotembelea. Unahakikishiwa kupata kitu kipya utakachopenda kila unapotembelea blog hii, Utapata makala za Kikatoliki, sala, Tafakari, Picha za Katoliki, nyimbo za Kikatoliki n.k. Kwa sasa kuna posti Mpya 1179 za Kikatoliki kwa ajili yako, nimekutayarishia kila kitu kazi yako ni kuperuzi na kutembelea Blog hii mara kwa mara.

Chagua unachotaka hapa…

|| MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa

Jina
Dini/dhehebu
Mfano Mwislamu, Katoliki, Lutherani, Mlokole n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako

Karibu tena na Mungu Akubariki

Nakutakia pasaka njema

ABOUT ME | MY PERSONAL BLOG

.