Kwa nini Binti usivae Suruali, ubaya wa Suruali kwa wanawake

KWANINI BINTI USIVAE SURUALI..!

By : Ntogwisangu J. C

🔹Kumekuwa na mada nyingi na maswali mengi kuhusu mabinti kuvaa suruali (hasa waliookoka), michango mingi na mafundisho mengi yametolewa, nami naomba niongezee kitu kidogo.

🔹Zifuatazo ni sababu kwanin binti hautakiwi kuvaa suruali…

👉HAISITIRI MWILI.!

🔹Neno la Mungu linaagiza wanawake wavae Mavazi yanayositiri (yanayofunika /yanayoficha Mwili) 1 Timotheo 2 :9

🔹Lakini vazi la suruali kwa mabinti halisitiri Mwili na badala yake yanauonesha /yanautangaza mwili uonekane vizuri. Hivyo hukiuka agizo la Mungu.

🔹Mwili wa mwanamke ni wa tahamani sana na haupaswi kuonekana ovyo hasa sehemu kama matiti, kiuno, kitovu na mapaja. Ingawa suruali inaweza isioneshe sehemu hizo lakini bado inauchonga mwili wa mwanamke na kuufanya usiwe siri tena bali uwe wazi.

🔹Vazi la suruali kwa mwanamke lilibuniwa ili kufanya umbile (shape) ya mwanamke lionekane vizuri na kuongeza mvuto /uzuri wa mwanamke, na wakasahau jukumu kubwa na la kwanza la Mavazi ni kuuficha mwili.

👉HUCHOCHEA UZINZI.

🔹Neno la Mungu linasema yeye amtazamaye mwanamke na kumtamani amekwisha kuzini nae moyoni Mwake, Mathayo 5 :28

🔹Mwanaume kwa asili ni mtu wa tamaa, hii haijalishi awe anamjua Mungu au la, kinachotofautiana ni uwezo tu wa kujizuia tamaa hiyo.

🔹Ndio maana mtumishi wa Mungu Ayubu aliwejiwekea msimamo kuwa hatamtazama mwanamke kwa kumtamani (Ayubu 31 :1)

🔹Sasa kwa vazi hilo kwa wanawake pamoja na Mavazi mengine yasiyositiri mwili yanawakosesha wangapi? Yanawafanya wangapi kuzini kila siku kwa tamaa ya macho?

🔹Neno la Mungu linasema mtu yeyote atakayemkosesha mwenzake kufanya dhambi na akamkosa Mungu, basi AFUNGWE JIWE SHINGONI NA ATUPWE BAHARINI. Dada kama kuna watu unawakosesha na kuwafanya wafanye dhambi HAKIKA HUKUMU YAKO IPO (Mathayo 18 :6-7).

👉SIO UTAMADUNI WETU WAKIAFRIKA.

🔹Utamaduni ni wa muhimu sana kuzingatiwa tunapojadili kuhusu swala la Mavazi. Hata biblia huheshimu tamaduni Za watu isipokuwa zile ambazo zipo kinyume na Neno la Mungu.

🔹Kwa Utamaduni wetu wa kiafrika hauruhusu mwanamke kuvaa suruali, mambo ya kuvaa suruali yamekuja miaka ya hivi karibuni kutokana na utandawazi na watu kuanza kuiga tamaduni Za kigeni (wazungu).

🔹Neno la Mungu linasema mwanamke asivae Mavazi yampasayo mwanaume na mwanaume asivae Mavazi yampasayo mwanamke.

🔹Kutokana na Utamaduni wetu ninaweza kusema, mwanamke asivae Suruali (vazi limpasalo mwanaume) na mwanaume asivae Sketi (vazi limpasalo mwanamke).

🔹 Ingawa kwa baadhi ya nchi kama Scottish wanaume walikuwa wanavaa Sketi, ila huo ndio ulikuwa Utamaduni wao sijafahamu kwa Sasa kama imebadilika.

🔹Utamaduni Inabidi uzingatiwe na si kuamini kila kitu cha Mzungu kipo sahihi.

  1. MZUNGU SIO MUNGU.

👉MAVAZI YANABEBA UTAMBULISHO.

🔹Vazi unalovaa linaweza kukutambulisha hata kama haujajitambulisha. Ukimuona Askari unaweza ukamtambua kutokana na vazi lake (uniform yake), Ukimuona daktari pia kwenye vazi lake la kazi bila hata kujitambulisha utamfahamu kama ni daktari. Je, vazi lako la suruali linakutambulishaje?

🔹Mithali 7 :10, "Na tazama, mwanamke akamkuta, ana MAVAZI YA KIKAHABA"

🔹Andiko hapo juu 👆linasema mwanamke ana Mavazi ya kikahaba, Je Mavazi ya kikahaba ni yapi? Nguo yoyote ile isiyositiri mwili kama Mungu alivyoagiza hiyo ni Nguo ya kikahaba.

🔹Nguo inayokuacha kifua wazi, kitovu, kiuno na mapaja wazi Nguo hiyo haijauficha mwili hivyo ni vazi la kikahaba. Yapo Mavazi mengi ya kikahaba na suruali ikiwa ni moja kati ya Mavazi hayo.

🔹Kama tulivyoona mtu aliyevaa vazi la kiaskari ni Askari, aliyevaa vazi la kidaktari ni daktari, vipi aliyevaa Mavazi ya kikahaba atakuwa ni nani?

🔹Ni aibu kwa mwanamke anayejiheshimu kuvaa nguo ya kikahaba . si kila kitu ni cha kuiga , mambo mengine muwaachie wenyewe.

  1. MAVAZI YA KIKAHABA NI KWA AJILI YA MAKAHABA, NA SI MWANAMKE ANAYEJIHESHIMU.

👉SURUALI SI VAZI LA HESHIMA KWA MWANAMKE.

🔹Katika Mavazi ya heshima kwa mwanamke suruali si vazi la heshima. Ingawa wanasema sijui kuna suruali Za kike na kujaribu kuzitetea Ibilisi ni Ibilisi hata akijifanya malaika wa Nuru.

🔹Kama suruali ni vazi la heshima kwanini wanawake wasilivae wanapoenda sehemu za heshima mfano msibani? Na hata kama wakivaa basi watajifunga na khanga juu yake.

🔹Kama suruali ni vazi la heshima kwanin usivae siku unayoenda kutambulishwa ukweni? Na badala yake unavaa Sketi ndefu mpaka miguuni tena na khanga juu, lakini cha kushangaza unaenda kanisani na kijisuruali kimekubana mpaka upindo wa Nguo ya ndani unaonekana.

  1. KAMA UNAHESHIMU UKWENI, SI ZAIDI NYUMBAN MWA MUNGU ❓

👉MAVAZI UNAYOVAA NI KWA AJILI YA WENGINE.

🔹Mavazi unayovaa si kwa ajili yako ila kwa ajili ya wengine. Kama Mavazi unayovaa ni kwa ajili yako kwanini usivae ile Nguo yako ya gharama unayoipenda siku ukiwa hauna ratiba ya kutoka halafu jioni ukaivua? Au siku utajayoalikwa kwenye sherehe usivae zile yeboyebo zako na ule mtumba wako ulionunua kwa mmachinga ukaenda nazo?

🔹Nguo nzur au mbaya ni vile watu wanavyoona na si wewe unavyoona, Nguo hata kama iwe nzur vipi kama watu wanaokuzunguka wakisema haikupendezi sidhani kama utaivaa.

🔹Suruali na Nguo unayovaa zisizositiri mwili hazikupendezi ila zina kudhalilisha, na kama mtu anakusifia kama unapendeza huyo hakutakii mema tena ni kipofu.

🔹Na kipofu akimuongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia kwenye shimo.

……..

👉NI WAPI NIVAE SURUALI ❓VAA SURUALI KAMA KAZI YAKO INAKUBIDI UVAE SURUALI, KAMA UNALALA, UKIWA UNASAFIRI SAFARI NDEFU ILA UJIFUNGE NA NGUO NYINGINE JUU NA MATUKIO MENGINE YANAYOKULAZIMU KUFANYA HIVYO.

👉USIVAE SURUALI KAMA FASHION UKIWA UPO KWENYE MIZUNGUKO YAKO YA KILA SIKU.

Mwl John Charles Ntogwisangu

(Youth Spiritual counsellor & Lecturer)

Watsap # 0712463344

.

.


images-21.jpeg
Ujumbe wangu kwako kwa sasa

Kwa njia ya sala Binadamu anampa Mungu Utukufu, Mungu anampa Binadamu Wokovu na Neema.

Mungu Akubariki sana… Tuombeane!

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.