Jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo katika dunia ya leo

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Tunaweza kusadiki vipi?

1- Ishi Kwa Kufuata Mfano Wa Mwokozi Yesu Kristo
Kwa Kuishika Amri Yake Kuu Ambayo ni Upendo. Mpende Bwana MUNGU wako kwa Moyo wako Wote, Mwili na Nafsi yako yote

Wasamehe Wanaokukosea, Na Uwapende Pia.

2. Kubali kua Una dhambi na Tubu Pia.

3. Soma Na Fuata Yaliyoandikwa katika Biblia.

Mathayo 4:4

_Naye Akajibu Imeandikwa, Mtu hataishi kwa Mkate Tu Bali katika kila neno litokalo katika kinywa Cha MUNGU._

Mkristo Silaha na Muongozo Wa Maisha yake Ni Neno La MUNGU Tu.

4. Muache MUNGU Akubadilishe. 🤗

Kuna Baadhi ya Tabia Ukiwa nazo ni Ngumu kuacha. Bali kwa Neema ya MUNGU tu.

Ezekiel 36

26-Nami nitawapa ninyi Moyo Mpya, Nami nitatia Roho Mpya Ndani yenu, Nami nitatoa Moyo wa jiwe, Nami nitawapa Moyo wa Nyama.

27-Nami nitatia roho yangu Ndani yenu na kuwaongoza katika sheria zangu, Nanyi Mtazishika Hukumu zangu na kuzitenda.

5 Elewa Kua Ni Lazma Utatengwa Na Kusulubiwa kwa Imani Yako..😊

Dini ya Ukristo Siku Hizi Imefanyiwa Standardisation.
Vitu Vingi Vilivyo Andikwa Katika Vitabu Vitakatifu Vimebatilishwa. Ukionekana Mkristo Ulie na Msimamo utapigwa Vita Tu.

Ila Usife Moyo kwani Ushindi ni Hakika.

2 Timothy 3:12
_Naam, na Wote wapendao kuishi Maisha ya Utauwa katika kristu Yesu Wataudhiwa._

6 Tenga Muda Wa kutosha Kufanya Maombi 🙏🏽

Fanya Maombi kwa Ajili yako Ndugu na Jamaa. Pia Watu Wasioweza kujiombea kama, Maadui, Watoto, yatima n.k.

Katika Waefeso 1:16

_Siachi kutoa shukrani kwa Ajili yenu nikiwambuka katika Wala zangu_

7 Jaribu Kufikiri na Kuona Mambo Katika Muono Wa Watu Wengine (point of view) hta kama Hukubaliani nao. 😀

Fanya Maombi kwa Ajili yao. Ili Waijue kweli Hyo ni kwa faida yao na yako pia.

8 Kua Mvumilivu kwa Wale Wanokukwaza, 🙂Unapokua mkristo Makwazo Ni sehemu ya Maisha.

Jifunze kuombea na kusamehe adui zako kama MUNGU anavofanya kwako..

9 Saidia Watu katika Shughuli Mbali Mbali za kujitolea. 🛠Itakujenga Kiroho na Kukuongezea Moyo Wa upendo.

10. Usiwe na Mashaka Wala kumkana MUNGU hta kama unapita katika Mapito Gani.*🙏🏽

11. Yaishi Yale Unayofundisha Wengine, ili nao pia Watamani kuishi Maisha ya kikristo.🙂

12. Jiunge na fellowship au Tafuta Marafiki Wa kutafakari nao Maandiko Matakatifu.👫

Hapa unatakiwa kuweka effort kujua Maarifa Mbali Mbali, pia Hao wawe Ndugu zako ktk Imani Unaweza Ukawaomba Msaada wa kiroho Muda Wote.

13.Usione Aibu Juu ya Imani yako. Tangaza wokovu Kila unapopata nafasi. 💪🏾

Marko 8:38

_Maana kila mtu Atayenionea haya Mimi na Maneno yangu katika kizazi hili cha Uzinzi na Dhambi, Mwana wa Adamu Atamuonea haya Atakapokuja katika utukufu wa baba yake pamoja na Malaika watakatifu._ 🤔

14. Jitahidi kuishi Maisha ya Kutokujionyesha.🙏🏽

15. Watendee Wengine kama unavotaka kutendewa 😊

16- Soma sana vitabu na machapisho Mbali Mbali ya kidini Kuongeza Ufahamu na Maarifa.✍🏽

17. Kua na Furaha Muda Wote* Kwani Moyo wenye Furaha ni Dawa kwa Mwili 💃🏽

*FINITO🙏🏽Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo katika dunia ya leo

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo katika dunia ya leo

a.gif Tafakari ya leo kuhusu Farao

NASHINDWA KUMUELEWA FARAO.
Ana Ufalme na Jeshi lote, mawaziri, wachawi na wanajimu, Mali zote na kila kitu na Ikulu iliyojengeka na kiti chake cha enzi, lakini ananyimwa usingizi na Waisrael ambao hawana chochote cha maana zaidi ya Neno na Ahadi juu yao… soma zaidi

a.gif Ujumbe wa leo

*UJUMBE WA LEO*
Ndege anapokuwa hai huwa anakula sana funza, lakini atakapokufa nae huliwa na funza.. Maisha yanabadilika kila wakati, usimdharau wala kumuumiza mtu yeyote katika maisha…Unaweza ukawa imara sana leo lakini kumbuka maisha ni imara kuliko wewe.., Mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima….. soma zaidi

a.gif Imani na mapokeo ya kanisa Katoliki kwenye Biblia

JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni Mwaminifu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Picha ya Yesu wa Huruma

mwili-utakaofufuliwa-ni-huu.JPG

a.gif Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo… soma zaidi

a.gif Neno "Amina" katika sala lina maana gani?

Neno "Amina" katika sala lina maanisha "Na iwe Hivyo" (Hesabu 5:22).. soma zaidi

a.gif Neema ya Utakaso yapoteaje?

Neema ya Utakaso yapotea kwa kutenda dhambi kubwa (dhambi ya mauti).. soma zaidi

a.gif Mipango ya Mungu

Mipango ya Mungu daima ni myema, Mungu anapanga Mema katika maisha ya mtu kama akifuata mapenzi yake. Tatizo ni kwamba watu wanafuata mapenzi yao wenyewe na kisha kukosa yale mema Mungu aliyopanga kwao… soma zaidi

a.gif Agano la Tohara

1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu… soma zaidi

a.gif Swali la kutisha

.. soma zaidi

a.gif Kwa nini ubatizo unafanyika kwa maji?

Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo ishara ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa nini?

Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa Mwili wa Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi padri anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai, Roho Mtakatifu anavigeuza kwa dhati: mkate si tena mkate, wala divai si tena divai, ingawa maumbo yanabaki yaleyale kwa hisi zetu… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu kifo

Makala kuhusu kifo;.. soma zaidi

a.gif Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha

Yesu ni Mwanga na Uovu ni giza.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.