Jifunze kitu kupitia mkasa huu wa kusisimua

By, Melkisedeck Shine.

Kulikua na bwana👤mmoja masikini sana😳😳Kutokana na dhiki kumwandama ilifikia wakati alitamani kufa😮kuliko kuendelea kuishi sehemu alipokuwa anaishi kulikuwa na
msitu🌵🌱🌿🌴🌲mkubwa ambao ndani yake linaishi zimwi👹👹👹lenye kula watu na katika msitu huo hajawahi kuingia binadamu👴 akarudi salama✌wote waliliwa na zimwi👹👹

Yule bwana👤aliona👀njia rahisi ya kifo ni kuingia msituni ili akaliwe na zimwi👹👹👹👹alifunga safari mpaka msituni alipofika tu alishangaa😮😮kujikuta amesimama mbele ya zimwi👹👹👹👹kubwa
lenye hasira kali😮lile zimwi kabla halijamtafuna yule bwana lilimuuliza hujasikia👂👂kuwa huku naishi mimi zimwi nakula watu👪?au wewe huogopi kuliwa?”👹

Yule bwana👤akajibu taarifa ninazo nimekuja huku unile na mimi nife😢maana sina raha ya
maisha zimwi👹👹akamuuliza una tatizo gani? mpaka useme huna raha ya maisha?”yule bwana👤akajibu umaskini na dhiki zimenizidi mnoo😳nimekata tamaa kwa ufukara nilionao.”

zimwi liliposikia👂👂hivyo lilimwangalia yule bwana👤kwa dakika kadhaa halafu likamwambia nisubiri hapohapo nakuja usijaribu kunyanyua mguu wako👣👣hata mara moja zimwi👹likatoweka baada ya muda mfupi lilirejea likiwa limeshika vipande viwili✌vya miche ya dhahabu likamkabidhi na kumwambia yule bwana👤umesema shida yako ni umaskini sasa chukua hizo za dhahabu zikawe utajiri wako ila siku ukirudi tena nakutafuna bila kukuuliza kitu chochote👹👹

Yule bwana akaondoka👣msituni akiwa haamini😮😮uku akijisemea bahati iliyoje unaenda msituni na unakutana na zimwi👹👹badala likutafune linakupa dhahabu za kubadilisha maisha yako😀😊😀😊
alijisemea yule bwana huku akitembea kwa hatua👣👣za haraka kuelekea nyumbani kwake akiwa na furaha sana😀😀😀😀😀😀😀

Alipofika nyumbani🏡kwake alipofungua tu mlango akamkuta malaika mtoa roho yupo ndani anamsubiri😮yule bwana👤akamuuliza umefuata nini hapa nyumbani🏡kwangu?malaika mtoa roho akamjibu mimi ni mgeni wako nimefuata roho yako😮siku zako za kuishi hapa duniani zimekwisha yule bwana alilalamika sana😳😳uku akisema mbona mimi sina bahati😳nimehangaika siku zote na umaskini
wangu leo nimepata dhahabu za kunifaa ili
niondokane na dhiki ndiyo siku zangu za kuishi
zinafika ukingoni😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢

Yule bwana👤akamwambia malaika mtoa
roho naomba siku mbili✌niuze hizi dhahabu, nipate pesa💰💰ili niwaagawie maskini wenzangu angalau wabaki na nafuu ya maisha,
umaskini unatesa sana😳nitajiskia vibaya😳😳 nikifa na kuacha hizi dhahabu humu ndani, halafu zije ziokotwe na tajiri wakati maskini wanateseka😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳

Aliposema maneno hayo malaika mtoa roho
alimwambia umesema jambo jema👍lenye
kumpendeza Mungu😀sadaka ni kitu kizuri sana basi nakupa hizo siku mbili✌malaika mtoa roho akaondoka👣zake yule bwana👤akafanya kama alivyoahidi aliuza zile dhahabu na kupata mamilioni ya pesa💰💰💰 akawazungukia maskini wale wenye dhiki na uhitaji mkubwa aliwagawia fedha zote💰💰💰

Baada ya siku mbili✌yule bwana👤alibaki nyumbani🏡akisubiri malaika mtoa roho aje kuchukua roho yake😢😢😢muda ulipofika malaika alitokea yule bwana akatabasamu☺kisha akasema kabla hujanitoa roho ningependa kujua Mungu amependa sadaka niliyotoa?malaika mtoa roho akamjibu: “Mungu amefurahi sana😀maana

umewasaidia watu maskini kubadili maisha yao na kwa furaha hiyo Mungu amekuongezea miaka mingine themanini(80)utakuepo kwenye hii dunia🌍na utapata mafanikio makubwa😀😀😀😀😀😀😀

Yule bwana👤akalalamika sana uku akisema usiniache naomba🙏uchukue roho yangu tafadhali nitaishi vipi na umaskini😳😳😳😳😳 huu?umeniacha nimegawa mali zangu💰💰zote ndipo unaniambia nitaendelea
kuishi sasa nawezaje kuishi na ufukara huu
ambao nilishaukatia tamaa😳😳😳?malaika mtoa roho wala hakutaka kumjibu alipaa zake.

Yule bwana👤aliwaza sana akajisema hawezi kuishi akaamua kurudi🏃msituni ili akaliwe
na zimwi👹na alipofika tu alijitupa miguuni👢mwa zimwi👹👹👹👹👹👹lile huku akilia😢😢😢na kusema nitafune nife sitaki kuishi tena😢😢zimwi akamwambia ni nini kilichokufanya uje hapa tena?nilikupa dhahabu na nikakwambia usirudi tena👹👹👹👹👹👹👹

Yule bwana alimsimulia zimwi👹kila kitu lile zimwi👹likaondoka tena na kurudi na miche miwili✌ya dhahabu akampa tena✊huku akasema hii ni mara ya mwisho usirudi tena✋na ukirudi sikuulizi kitu nakutafuna
moja kwa moja bila ya kukuuliza chochote👹👹

Yule bwana👤alipokea ile miche ile ya dhahabu kwa wasiwasi😮alipokuwa anatoka msituni, aliamini akifika nyumbani🏡angekutana na malaika mtoa roho😳alifungua mlango kwa tahadhari lakini hakumkuta mtu alikaa kusubiri labda angetokea lakini haikuwa hivyo asubuhi🌞ya siku iliyofuata alikwenda kuuza
zile dhahabu akapata fedha nyingi💰💰sana akafungua miradi mbalimbali ambayo ilimpa faida nyingi ndani ya nda mfupi akawa tajiri mkubwa sana💰💰💰💰💰💰💰💰💰💰💰💰

siku zote aliishi vizuri na watu👪aliukumbuka
umaskini wake wa zamani😳akawa mtoa✊✊ sadaka mzuri kwa maskini😀alifanya ibada👍 huku kichwani akikumbuka ahadi ya miaka themanini 80😀😀 Na ilipowadia malaika mtoa roho alimtokea😮😮😮 na kutimiza ahadi yake ya kuchukua roho yake😢😢😢😳😢😳😢😳😢

,,,Roho ya mtu mwema👍👍ilitoka taratibu, huku malaika mtoa roho akimbembeleza
na kumliwaza ili asipate kusikia uchungu wa roho unavyouma😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳😳

tupendane💕tuheshimiane👍tusaidiane✊tukumbushane😊tukatazane mabaya✋tuamrishane mema👍na tuwe ni wenye kutoa ata kwa ivi vidogo tulivyonavyo😉Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Jifunze kitu kupitia mkasa huu wa kusisimua

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Jifunze kitu kupitia mkasa huu wa kusisimua

a.gif Mungu akipanga kukuinua hakuna anayeweza kukushusha

MKASA WA KUSISIMUA : MUNGU AKIPANGA KUKUINUA HAMNA ATAEWEZA KUZUIA, HATA SHETANI HATOWEZA… soma zaidi

a.gif Nafasi ya Bikira Maria Katika Kanisa Katoliki

Kanisa katoliki linamthamini Bikira Maria kama Mama wa Mungu, Mama wa Kristu, Mama wa Mkombozi pia Mama wa uhai kuna maneno kadhaa hutumika pia kufafanua zaidi hiyo heshima mfano HYPERDULIA zaidi ya…. Bikira Maria tunamheshimu zaidi ya watakatifu, PROTODULIA ikiwa na maana ya heshima kwa Bikira Maria zaidi ya Mt. Yoseph na pia LATRIA likiwa na maana ya heshima kwa Mungu peke yake kwani ndani yake kuna kunakuabudu pia!!!.. soma zaidi

a.gif Mungu ni Mkubwa kiasi gani

Mtoto mmoja alimuuliza baba yake. "Baba, hivi Mungu ni mkubwa kiasi gani?" Baba yake akatazama juu angani akaona ndege ya abiria akamuuliza mwanae "mwanangu, ile ndege ina ukubwa Gani?" Mtoto akajibu ni ndogo sana.
Basi Baba yake akamchukua hadi uwanja wa ndege walipofika karibu na ndege akamuonesha ndege akamuuliza " ile ndege ina ukubwa gani?? Mtoto akajibu "Hiyo Ndege ni Kuuuubwa sana" basi Baba yake akamwambia.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Kanuni ya imani

[Wimbo Mzuri PA.gif] Salamu Maria Salamu

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala ni chakula cha roho

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

UJUMBE-WA-ZA-JIONI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Biblia iliandikwa kwa kusudi gani?

Biblia iliandikwa kusudi tupate “kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini” tuwe “na uzima wa milele” (Yoh 20:31)… soma zaidi

a.gif Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi tufanye nini?

Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi: Tumwabudu,tumshukuru, tumwombe kwani yeye ni Mwenyezi. (Mt 2:11, Lk 17:11).. soma zaidi

a.gif Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?

Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake mafumbo hayakuadhimishwa vizuri… soma zaidi

a.gif Tumekatazwa nini ili tulinde usafi wa moyo?

Tumekatazwa haya;.. soma zaidi

a.gif Ni nani ampaye padri Daraja la Uaskofu?

Ni Baba Mtakatifu pekee au humteua Askofu mmoja akisaidiwa na maaskofu wengine wawili humweka wakfu Padri huyo kuwa Askofu (Mt 13:2-3).. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Daraja ndiyo nini?

Sakramenti ya Daraja ndiyo Sakramenti ambayo mwanamme mkatoliki aliyeitwa na Mungu hupata mamlaka na neema ya kuendeleza ndani ya Kanisa Utume Kristo aliowakabidhi Mitume wake.. soma zaidi

a.gif Malaika wote walidumu katika hali njema na ya heri?

Siyo, Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, Wakatupwa Motoni… soma zaidi

a.gif Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo… soma zaidi

a.gif Mapokeo ya Mitume ndiyo nini?

Mapokeo ya Mitume ndiyo yale yote ambayo Yesu aliwakabidhi Mitume wake, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu yatadumu hata mwisho wa dunia katika mafundisho, liturujia na maisha ya Kanisa… soma zaidi

a.gif Sodoma na Gomora

Mwanzo 18:16-33, 19:1-29.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.