Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

By, Melkisedeck Shine.

Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.

“Kuna vitu sita unatakiwa uvitambue, “ Aliiambia penseli,

“Kabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.”

Alisema muumbaji wa penseli.

“Moja,” alianza kuvitaja,”utakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wako”

“Mbili” aliendelea kutoa nasaha, “utapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.”

“Tatu, utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya.”

“Nne, kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika.”

“Tano” alisisitiza mtengenezaji penseli, “kwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki.

“Na sita”, alimalizia muumbaji yule wa penseli, “ipo siku utaisha na kupotea. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu uliombiwa kuufanya”

Penseli ilielewa na kuahidi kukumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.

Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.

Moja, una uwezo wa kufanya mambo mengi na makubwa, kama utajiweka kwenye mikono ya Mungu.

Mbili, utakutana na magumu mengi ya kuumiza, lakini hayo ndiyo yatakufanya uwe mtu imara na bora, usiyakimbie.

Tatu, una uwezo wa kurekebisha makosa yote uliyoyafanya. Usijilaumu.

Nne, sehemu yako ya muhimu ni ile iliyo ndani yako kwani ndiyo inayoandika maisha yako. Ilinde.

Tano, kila sehemu utakayopita, acha alama yako kwa kufanya mazuri yatakayokufanya ukumbukwe daima, bila kujali mazingira. Timiza wajibu wako kwa kiwango cha juu.

Sita, tambua kuwa ipo siku utakufa. Usiwe na hofu yoyote juu ya kifo kwani ukiogopa kifo hutafanya lolote hapa duniani.

Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumba wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza dhamira uliyotumwa na Muumba.

UBARIKIWE SANA.Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

a.gif Tafakari ya SA-SE-SI-SO-SU

:::::"SA"::::::
:::::::"SE"::::::
:::::::::"SI"::::::
::::::::::"SO"::::::
::::::::::::"SU"::::::.. soma zaidi

a.gif Maneno ya busara kwa anayetafuta Mme au Mke

Usifanye maamuzi kwa kutumia vigezo vyepesi.
"Nampenda sana"
"Tunapendana mno"
Unaweza kumpenda mtu yeyote. Upendo huzaliwa na huuawa na mazingira fulani. Kwamba unampenda (sana) sio jambo la msingi… soma zaidi

a.gif Chagua kunyamaza: Huu ni ushauri kwa Leo

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Sali daima

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu John Fisher

Mama-Bikira-Maria.jpg

a.gif Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?

Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha "Mungu Mtawala".. soma zaidi

a.gif Nani ni Mitume wa Mataifa?

Mitume wa mataifa ni Paulo na Barnaba.. soma zaidi

a.gif Dhambi za uchafu huleta hasara gani?

Huleta hasara hizi;.. soma zaidi

a.gif Huruma ya Yesu Kristo kwa mwenye dhambi

Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio wakati ambao Yesu anakua karibu na mtu sana hata kuzidi wakati mwingine wowote.
Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio Yesu anakua karibu zaidi, lakini tatizo ni kwamba huo ni wakati ambao mtu hawezi kutambua uwepo wa Yesu. Neno moja tuu la Matumaini na Upendo wakati huo linaweza kumfungua mtu na kumbadilisha… soma zaidi

a.gif Kilindi cha Huruma ya Mungu

Habari njema ni kwamba Yesu sasa anakuja kwako Kama Bwana wa Huruma, Mwalimu na Rafiki Mwema Akupendaye, Angalia Usichelewe Wakati akija Kama Hakimu asikukute bado huna ushirika nae na hujui haki na hukumu yake. Wakati ndo huu wa kukimbilia Huruma na Upendo wake wa Bure Kwako... soma zaidi

a.gif Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20).. soma zaidi

a.gif Kwa ajili gani Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu?

Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu kwa ajili yetu wanadamu na wokovu wetu ili atupatanishe na Mungu na kutushirikisha tabia ya umungu. (2Pet, 1:4).. soma zaidi

a.gif Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?

Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo.. soma zaidi

a.gif Majilio ni nini?

Majilio ni kipindi cha Dominika nne cha kujiandaa na Sherehe ya Kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo, yaani NOELI… soma zaidi

a.gif Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni nini?

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.