Hadithi: Mkasa wa kusisimua, Jifunze kitu hapa

By, Melkisedeck Shine.

Watu wawili👬 walikuwa wanakunywa pombe🍺🍻 baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana🙅🏾‍♂ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.

Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.

Kumbe amemwua mwenzie.😰

Ndipo alipoanza kukimbia🏃🏾 huku shati laki likiwa limechafuka sana na damu. Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza.
🏃🏾 🏃🏿‍♀🏃🏾🏃🏿‍♀🏃🏾🏃🏿‍♀🏃🏾

Huyu mwuaji akakimbilia kwenye 🏡🏃🏾nyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza.

Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?😨

Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha. Yule mcha Mungu akavua shati👔 lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa.

Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue. Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia🏃🏿‍♀🏃🏾🏃🏿‍♀🏃🏾🏃🏿‍♀🏃🏾🏃🏾🏃🏿‍♀🏃🏾🏃🏿‍♀🏃🏾 na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.

Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi👮🏾👮🏽‍♀ na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa👴🏼 kwa kumwua mtu mwingine.

Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana😞 akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru.

Hakimu⚖ akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa.

Alilia😭😩 sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.😰

Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu _*"LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE."*_

Wapendwa,
YESU alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu. Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki. YESU aliuawa kwa kosa lako na langu. Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu.

Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.

Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu. Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea.

Wapendwa,
*Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?*

T A F A K A R IFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Hadithi: Mkasa wa kusisimua, Jifunze kitu hapa

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Hadithi: Mkasa wa kusisimua, Jifunze kitu hapa

a.gif Wakati unapitia magumu usikate tamaa

Kuna Kipindi katika maisha yako unaweza ukapitia mambo Fulani magumu hadi ukaanza kujiuliza,hivi kwa nini yote haya yananitokea?Why Me God?.Na Mimi nimeshawahi kupitia katika hali hii… soma zaidi

a.gif Historia Fupi ya Ibada ya Rozari

Katika Kalenda ya Kanisa Katoliki,
huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi
ni miezi ambayo imewekwa kwa ajili ya
Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo
hiyo miezi huwa inasaliwa rozari.
Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa
nini ifanyike miezi hiyo? Yafuatayo nimajibu, mwezi wa tano umewekwa kwa
heshima ya Bikira Maria kutokana na
nini kilitokea katika historia hapo
nyuma… soma zaidi

a.gif Siri ya kamba nyekundu

Miaka zaidi ya 3000 iliyopita katika mji wa Yeriko alikuwepo mwanamke mmoja kahaba, jina lake Rahabu. Huyu mwanamke aliwaokoa wapelelezi wa Israel waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi ktk nchi yao… soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA KUTUBU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mama wa Mkombozi

[Tafakari ya Sasa] 👉Njia ya Kumtafuta Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Brigita wa Sweeden

MARIA-WOKOVU-WETU.JPG

a.gif Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho

FROM FR TITUS AMIGU
Siku moja, miaka kama 14 hivi iliyopita, nilimzingua mchungaji wa kikanisa fulani. Alinijia mbio na kuniambia, "Ati… Kadinali wenu amesema kuwa pombe sio dhambi! Kwanini usihame huko? Angalia sasa, hata kiongozi wenu wa juu wa Kanisa amekosea kwa kusema pombe sio dhambi.".. soma zaidi

a.gif Mtume Thoma

Thoma au Didimo, yaani Pacha alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu, kwa namna ya pekee na Wakristo wa maeneo yaliyokuwa mashariki kwa Dola la Roma, kuanzia Iraq hadi India… soma zaidi

a.gif Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?

Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake… soma zaidi

a.gif Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie nini?

Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie utakatifu na ukweli, si uzuri tu. Zisiigeuze kamwe kuwa igizo wala tamasha, kwa kuwa lengo si kuchangamsha watu bali kumtukuza Mungu… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Biblia

Kuhusu Biblia, Soma Maswali haya;.. soma zaidi

a.gif Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba

Chukua Hii
Yaweza
Kukusaidia.. soma zaidi

a.gif Nini maana ya neno "Fumbo"?

Fumbo ni ukweli ambao hatuwezi kuelewa kikamilifu, lakini tunasadiki kwa kuwa Mungu hutufumbulia. (Math 11:27).. soma zaidi

a.gif Je, Yesu alirudia maisha ya duniani?

Hapana, Yesu hakurudia maisha ya duniani: tofauti na watu aliowafufua warudie maisha haya, Yesu mfufuka ameshaingia utukufu wa milele:.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ni nini?

Sakramenti ni ishara wazi ionekanayo ya neema isiyoonekana, iliyofanyizwa kwanza na Yesu Kristu mwenyewe; ilete neema au izidishe neema moyoni mwetu… soma zaidi

a.gif Vilema ni nini?

Vilema ni mazoea ya kutenda mambo mabaya na kuacha kutenda mambo mema. (Gal 5:19-21).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.