Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

Angalizo; Tunapoongelea kuhusu pombe sio kwamba tunahamasisha kutumia pombe bali tuelewe kile tunachofanya kwa mapenzi ya Mungu!
pombe haikukataliwa ila itumike kwa kiasi.

Mhubiri 9:7
Wewe enenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.

Tito 2:3
Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;

1Timotheo 5:21,23
"21 Nakuamuru mbele ya Mungu, mbele ya Kristo Yesu na mbele ya malaika watakatifu, uyazingatie maagizo haya bila kuacha hata moja, wala kumpendelea mtu yeyote katika kila unachotenda.

23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.

Yoshua Bin Sira 31:25-29
"25 Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa pombe, maana imewaangamiza wengi.
26 Tanuru hupima ugumu wa chuma, na pombe hupima mioyo katika shindano la wenye kiburi.
27 Pombe ni kama uhai kwa mtu akinywa kwa kiasi, Maisha yafaa nini bila pombe?
Imeumbwa iwafurahishe watu.
28 Kunywa pombe kwa wakati wake na kwa kiasi, kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
29 Lakini kunywa pombe kupita kiasi, kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha."

Wakolosai 2:16-18a

"kwa hiyo basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu VYAKULA au VINYWAJI, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au sabato.

17 mambo ya namna hiyo ni kivuli cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye kristo.

18 msikubali kuhukumiwa na mtu anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee…."

Luka 7:31-35
"31 Yesu akaendelea kusema, "Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani?

32 Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine:
'Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza!
Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!'

33 Kwa maana Yohane alikuja, akawa anafunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: 'Amepagawa na pepo!'

34 Naye mwana wa Mtu amekuja anakula na kunywa, nanyi mkasema:
'Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi!'

35 Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali."

#Note; mvyinyo itumike kwa kiasi, kama huwezi kutumia kwa kiasi, ni afadhali kuacha kabisa.Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?

a.gif Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha

Yesu ni Mwanga na Uovu ni giza.. soma zaidi

a.gif Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili

Matayo 7:12;
"Basi yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.".. soma zaidi

a.gif Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki

Uzinzi na uasherati wakati huu umekuwa ndio sumaku kuu ya kuwanasa watu ili waende jehanamu… soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwema

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Anna

KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG

a.gif Uchaji wa Mungu ni nini?

Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake… soma zaidi

a.gif Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?

Nyaraka za Mitume ni;
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike.. soma zaidi

a.gif Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao… soma zaidi

a.gif MPANGILIO WA KURASA ZA POSTI NA MAKALA

Makala kuu za Wakatoliki;.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Watakatifu ndani ya Kanisa Katoliki

Soma haya kuhusu watakatifu;.. soma zaidi

a.gif Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala.. soma zaidi

a.gif Ndoa imewekwa na nani?

Ndoa imewekwa na Mungu mwenyewe na Yesu Kristo ameeinua na kuifanya Sakramenti. (Mwz 2:18; Mt 19:1-12).. soma zaidi

a.gif Dhamiri adilifu ni nini?

Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu.. soma zaidi

a.gif Amani ya Moyoni au Rohoni

Amani ya Moyoni au Rohoni ni hali ya kutokua na wasiwasi na hofu moyoni kuhusu Mambo ya Rohoni na ya kidunia… soma zaidi

a.gif Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.