IMG_20181021_135706.jpg

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kupanda na kutunza miti na misitu kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kampeni hii inaamini kuwa miti na misitu ikitunzwa vizuri inaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho.

Kampeni hii inafundisha kwamba miti na misitu inatakiwa ipandwe na iliyopo itunzwe ili iendelee kuwepo kwa miaka hii ya sasa na miaka ya baadae kwa kuwa miti na misitu ndio nguzo kuu inayoshikilia uhai wa wanyama waishio duniani wakiwemo watu.

IMG_20181021_134826.jpg

Kwa njia ya utunzaji wa miti na misitu, kizazi cha sasa cha watu na kizazi cha baadae kitanufaika kwa faida zitokanazo na miti na misitu.

IMG_20181021_134942.jpg

Hivyo basi, unaalikwa kupanda na kutunza miti na misitu ili iendelee kuwepo sasa na kwa miaka ijayo.

IMG_20170703_130425.jpg

Nini Maoni yako Kampeni hii?

Nitumie maoni au mapendekezo yako kuhusu kampeni hii hapa

Jina lako (majina)
Kampuni au Taasisi
Acha nafasi kama huna.
Namba yako ya simu
Email
Maoni au Ujumbe

Huduma na kampeni nyingine

Huduma na kampeni za sasa ni kama ifuatavyo;