IMG_20180108_172002.jpg

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Shine mwaka 2018.

Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia kulea na kuwakuza watoto yatima kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.

Kampeni hii inaamini kuwa watoto yatima kama walivyo watoto wengine nao ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae. Japokuwa hawana (wazazi) watu/mtu rasmi wa kuwatunza haimaanishi kuwa hawawezi kuwa watu wa maana baadae.

Kampeni hii inahamasisha watu wote kutunza, kuelimisha na kuwaelekeza watoto yatima katika malezi mazuri kimwili, kiroho, kiafya, kijamii na kielimu ili waweze kukuwa katika msingi mzuri utakaowafanya waweze kuendeleza au kuboresha maisha ya hapo baadae kwa kuwa watoto wa leo ndio watu wazima wa kesho.

images-9.jpeg

Kujenga msingi mzuri kwa watoto yatima kutadumisha na kuboresha maisha ya baadae.

IMG_20180125_205713.jpg

Hivyo basi, unaalikwa kusaidia kulea watoto yatima katika maongozi mazuri ili waweze kuwa watu bora hapo baadae na waweze kuwa msaada kwa kizazi cha sasa na kizazi cha baada yao.

SOKOINE-UNIVERCITY-OF-AGRICULTURE.jpg

Nini Maoni yako Kampeni hii?

Nitumie maoni au mapendekezo yako kuhusu kampeni hii hapa

Jina lako (majina)
Kampuni au Taasisi
Acha nafasi kama huna.
Namba yako ya simu
Email
Maoni au Ujumbe

Huduma na kampeni nyingine

Huduma na kampeni za sasa ni kama ifuatavyo;