Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Tarehe 15/05/2012 na Melkisedeck Leon Shine.
Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Umoja bila kuangalia tofauti za imani zetu za kidini.

Kama wewe unaamini kwamba wewe umeumbwa na Mungu wako, katika imani yako. Je watu wengine wasiokuwa wa Imani yako wenye kufanana na wewe kimaumbile wameumbwa na nani? Kwa hiyo kwa nini ujenge chuki juu yao na wakati wewe na wao ni sawa?

Wote ni Binadamu, kwa nini mchukiane? Sio kazi yetu kuhukumu wengine kuwabeza na kuwadadisidadisi au kuwazarau.

Kazi yetu kuu ni kuhakikisha kama inawezekana kuwafanya wenzetu wafuate njia ile tunayofuata kwa maana tunaamini ni ya kweli.

Katika Imani zote tunafundishwa kuwa tunawajibu wa kueneza Imaniyetu kwa wengine ili wao wawe sawa na sisi na sio kujengeana chuki kwa ajili ya Imani zetu.

Huwenda yule unayemjengea chuki ungemwendea kwa amani angekuelewa na angefuata Imani yako na hivyo ungekua umemsaidia na kumjenga.

Tuwe na Amani na tuelekezane taratibu, tusijenge chuki kati yetu, tushikamane na tuwe kitu kimoja huku tukisaidiana katika ulimwengu huu mmoja.

Kumbuka chuki inaanza pale tunapoanza kudadisiana, kubishana bishana, kuzarauliana na kujiona bora kuliko wengine. Tusifanye mambo kama haya. Kila mtu na aishike Imani yake mwenyewe kwa maana ni sahihi. Usichunguze na kukwaza wengine maana kwao pia ni sahihi kama unavyoona ya kwako.

Tusitengeneze wala kuruhusu mazingira ya kukwazana kwa kuepuka kufanya mambo yanayowakwaza wengine na hasa kutoa maneno yanayowakwaza wengine. Tumpe kila mmoja uhuru wake na tutakuwa na Amani na Upendo.

Kila mtu aishi anavyojisikia, anavyotaka na anavyoamini kwa njia hii tutakuwa na Amani.

Tusalimiane na tushirikishane mabo mengine ya kimaisha bila kujali Imani zetu tukijua tuu sisi tuu wanadamu tulio sawa, kwa hiyo tupendane na tuwe na umoja.

Nini Maoni yako Kampeni hii?

Nitumie maoni au mapendekezo yako kuhusu kampeni hii hapa

Jina lako (majina)
Kampuni au Taasisi
Acha nafasi kama huna.
Namba yako ya simu
Email
Maoni au Ujumbe

Huduma na kampeni nyingine

a.gif Kampeni ya kutetea watoto

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kuwakuza watoto kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae… soma zaidi

a.gif Kampeni ya usafi Binafsi

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kudumisha usafi wao binafsi kwa afya zao na kwa maendeleo yao.
Kampeni hii inaamini kuwa usafi wa mtu binafsi unamkinga na matatizo yatokanayo na uchafu kijamii na kiafya kwa mfano maradhi ambayo yanaweza kumzuia kuendelea na kazi zake za kawaida na kukua kimaendeleo kama mtu binafsi… soma zaidi

a.gif Kampeni ya kutetea watu wenye ulemavu

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea watu wenye ulemavu kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya walemavu wenyewe na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watu wenye ulemavu wanayo haki na nafasi sawa kama watu wengine katika jamii. Vile vile wanatamani kuishi kwa amani na furaha kwa hali ya kawaida kama watu wengine. Kwa hiyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza akawawezesha kuishi kwa furaha na matumaini kama watu wengine… soma zaidi

a.gif Kampeni ya utunzaji wa vyanzo vya maji

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza vyanzo vya maji kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa vyanzo vya maji vikitunzwa vizuri vinaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… soma zaidi

a.gif Kampeni ya utunzaji wa miti na misitu

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kupanda na kutunza miti na misitu kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa miti na misitu ikitunzwa vizuri inaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… soma zaidi