Kampeni Wa Wafanye Watabasamu

Let Them Smile Campaign

.

SMILE.gif

Utangulizi

Let Them Smile Compaign au Kampeni ya Wafanye nao Watabasamu ni kampeni endelevu ya kuhamasisha ushirikiano, umoja na kusaidiana katika jamii kwa watu wa matabaka yote.

Kampeni hii ina lengo la kuibua na kueneza furaha itokanayo na umoja na mshikamano kwenye jamii kwa njia ya kusaidiana na kushirikiana kimawazo, kwa matendo na kifedha.

images-7.jpeg

Kampeni hii imeanzishwa na Melkisedeck Leon Shine Disemba 2015 kama kampeni binafsi na kushirikishwa rasmi kwa uma Julai 2017.

images-9.jpeg

"Natamani watu wakumbuke kuwa vile unavyojisikia unapokuwa na shida au changamoto ndivyo vivyo hivyo mtu mwenye mahitaji/maskini anavyojisikia…Mfano unavyosikia njaa na kujisikia vibaya fikiri ni jinsi gani mtu anavyojisikia anapokaa na njaa siku zote ambaye yeye ni binadamu kama wewe…Vile unavyotamani kuwa na furaha katika Maisha ndivyo na Wengine wanavyotamani."

Kampeni ya Wafanye nao Watabasamu inawahamasisha watu wawe chanzo cha furaha kwa Wengine hasa wahitaji na wasiojiweza.

.

Nia au Malengo ya Kampeni Hii

1. Kuleta furaha na matumaini ya kuishi kwa watu hasa wenye mahitaji muhimu kama vile watoto yatima wasio na tegemeo, masikini na wasiojiweza kwa kuwasaidia moja kwa moja au kuwaongoza kukabiliana na changamoto zao. Mfano kwa Fedha, maneno ya faraja na uwepo wakati wa changamoto.

2. Kuleta amani katika jamii kwa kudumisha ushirikiano na upendo baina ya wenye nacho na wasiokuwa nacho.

3. Kudumisha ushirikiano na umoja kwa kujumuika pamoja katika shida na raha.

4. Kuleta maendeleo ya kizazi hiki na kijacho kwa kujenga msingi mzuri wa maisha.

.

Walengwa wa Kampeni

Watu wote ni walengwa wa kampeni hii kwa maana kila mtu anaishi na wahitaji kando yake katika maisha ya kawaida ya kila siku.

Kila mtu kwa nafasi yake anaalikwa kutoa Misaada ya hali na mali pamoja na Kujumuika katika shida na raha kwa maneno na matendo.

.

Unachoweza kukifanya kwa Sasa kuitikia kampeni hii.

Kampeni kwa sasa inahamasisha watu kwa njia ya mtandao kujiunga nayo kwa kufanya vile vilivyotajwa hapo juu kama nia kampeni hii.

Unaweza ukajiunga au ukaitikia wito wa kampeni hii kwa kufanya haya yafuatayo unapoweza;

1. Kutowapa kisogo wahitaji pale unapoweza.

2 Kumsaidia mhitaji kwa mawazo, matendo au fedha.

3. Kusaidia watoto yatima au wale wanaoishi katika mazingira magumu. Unaweza kusaidia mahitaji ya shule au chakula. Mfano unaweza ukampa mtoto chakula cha mchana pale unapomkuta na sio lazima kila siku.

4. Kujumuika na kuwasaidia wahitaji wanapokuwa katika changamoto za maisha kama Magonjwa, misiba nakadhalika.

.

Nini Maoni yako

HAPPY-MOMENTS.jpg

Nitumie maoni au mapendekezo yako kuhusu kampeni hii hapa

Jina lako (majina)
Kampuni au Taasisi
Acha nafasi kama huna.
Namba yako ya simu
Email
Maoni au Ujumbe
images-20.jpeg

Nitafurahi kusikia kutoka kwako maoni yako kuhusu kampeni hii

MAWASILIANO | ABOUT AUTHOR