IMG_20180109_192023.jpg

Misemo yangu ya leoπŸ‘‡

Karibu usome misemo mipya bora ya siku. Unaweza kusoma misemo mipya kila saa unapotembelea ukurasa huu. Tembelea ukurasa huu kila mara uwezavyo. Unahakikishiwa kusoma kitu kipya.

.

C.gif "Huwezi kuona thamani ya kitu ambacho hujakigharamia. Faida haina thamani kama haijagharamiwa." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Huwezi kusema unampenda Mungu usiyemuona kama huwapendi watu wale unaowaona. Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Vile unavyotaka akutendee mtendee vivyo hivyo." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Sala siyo maneno mazuri, bali sala ni NIA ya Upendo iliyobebwa na maneno mazuri. Tusali kwa kunuia kutoka moyoni na sio kwa kunena maneno tuu mdomoni." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Kama vile moto unavyozimwa na maji ndivyo vivyo hivyo hasira inamalizwa na maneno ya upole." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Ukitaka kupata amani, tumaini katika Ahadi za Mungu. Ahadi ya Mungu ni hii "Hatoacha kutusaidia wala kututupa"." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Usifadhaike moyoni pale unapokuwa katika matatizo au unapopitia changamoto katika maisha. Kumbuka kuwa Mungu yupo, anayaona hayo na anataka kukusaidia, ni wewe tuu kumpa nafasi ya kukusaidia. Hatumpi Mungu nafasi pale tunapozani tunaweza wenyewe." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Uzuri wa kitu huvutia MACHO lakini ubora wa kitu huuteka MOYO daima. Uzuri haudumu." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Hakuna Binadamu anayemchukia Mungu kama hajichukii yeye mwenyewe na wale wanaomzunguka. Huwezi kusema humtaki Mungu kama hujichukii mwenyewe na wale waliokuzunguka vivyo hivyo huwezi kusema Unampenda Mungu kama hupendi wengine waliokuzunguka." T.gif

AckySHINE.com

.

C.gif "Hakuna kitu cha Muhimu zaidi Duniani kama kumjua Mungu na kumuishi Mungu. Kila binadamu ameumbwa kwa ajili hii. Na Mungu anachotaka ndicho hichi, kumjua na kumuishi. Mengine yote ni maziada. Ukimuishi Mungu atakufanikisha katika yote." T.gif

AckySHINE.com

.